Loading...

Mchungaji ashushiwa kipigo na waumini wake Katavi


Mchungaji wa Kanisa la Sauti ya Uzima anayefahamika kwa jina la Nabi Elia mwenye umri wa miaka 36 amejikuta akinusurika kifo baada ya nyumba yake kuvamiwa na kushambuliwa kwa mawe na watu wanaotajwa kuwa ni waumini wa kanisa hilo ambao walimtuhumu kuwa ni mshirikina.

Taaarifa zimesema kuwa mchungaji Elia alivamiwa mtaa wa Kazima Ringini, Manispaa ya Mpanda alipokuwa akitoa huduma hiyo ya kiroho na kuponya waumini wake kwa zaidi ya miaka 6.

Akizumngumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Damas Nyanda amesema kuwa waumini watano wametiwa mbaroni na watu kadhaa kutokana na kitendo cha kujichukulia sheria mkononi.

Kamanda Nyanda amesema chanzo cha tukio hilo ni imani za kishirikina baada ya taarifa kuzagaa kuwa Nabii huyo alikuwa ameweka ‘misukule’ watano nyumbani kwake ambao waumini wa kanisa hilo walimtaka awatoe hadharani.

Waumini waliokamatwa ni William Kaluzi (19), Steven Alfred (31), Nicholaus Shadrack (33) na Tekla Didas (17)

Wengine waliokamatwa ambao si waumini wa kanisa hilo ni pamoja na Mashaka Moshi (23) mkazi wa Mtaa wa Nsemulwa na Faraja Hussein (22) mkazi wa Mtaa wa Kazima.

Chanzo: Eatv
Mchungaji ashushiwa kipigo na waumini wake Katavi Mchungaji ashushiwa kipigo na waumini wake Katavi Reviewed by Zero Degree on 12/04/2018 11:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.