Loading...

Amchinja mwanafunzi kisa pete


JESHI la Polisi Mkoani Kilimanjaro linamshikilia Kereto Likoko (Mmasai) kwa madai ya kumuua Mwanafunzi Samson Conrad aliyekuwa akisoma katika Chuo cha Faraja kwa kumkata na sime shingoni kwa madai ya kushindwa kumlipa fedha ya pete ambayo alikuwa akiuza.

Akizungumza jana Jumatatu Februari 11, 2019, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Kamanda Isah amesema taarifa za awali zinaonyesha kuwa kabla ya kifo marehemu akiwa na mwanafunzi mwenzake, Andrew Charles, walikuwa katika mazungumzo ya kuuziwa pete na mtuhumiwa huyo.

“Wakati wakiendelea na mazungumzo hawakuelewana na mtuhumiwa akitaka kupatiwa fedha yake, na alichomoa sime na kumjeruhi marehemu shingoni. Alivuja damu nyingi na amefariki dunia,” amesema

Chanzo: GPL
Amchinja mwanafunzi kisa pete Amchinja mwanafunzi kisa pete Reviewed by Zero Degree on 2/12/2019 07:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.