Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumanne Februari 12, 2019
Mshambuliaji wa Juventus raia wa Argentina Paulo Dybala, 25, anakaribia kufikia makubaliano ya kuhamia Real Madrid mwishoni mwa msimu.
Manchester United wameingia kwenye kinyang'anyiro cha kumsajili kiungo wa Paris Saint-Germain Adrien Rabiot, 23,mwishoni mwa msimu.
Barcelona walitaka kumsajili beki wa kati wa Fenerbahce Martin Skrtel, 34, wakati wa dirisha la usajili la mwezi Januari, lakini beki huyo kisiki wa zamani wa Liverpool aliktaa ofa ya miamba hao wa Uhispania. (AS)
Mustakabali wa Maurizio Sarri kama kocha wa Chelsea utaamuliwa ndani ya wiki mbili zijazo. (Telegraph)
Wachezaji wa Chelsea walifanya kikao maalum cha 'kurekebishana' katika uwana wao wa mazoezi wa Cobham jana Jumatatu kufuatia kipigo walichopata cha 6-0 dhidi ya Manchester City. (Mail)
Frank Lampard |
Beki wa Tottenham Juan Foyth, 21, amefichua kuwa alikataa kujiunga na klabu ya Paris Saint-Germain tili ajiunge na Spurs mwaka 2017. (Goal)
Barcelona wamefikia makubaliano na klabu ya Eintracht Frankfurt kumsajili streka wao raia wa Serbia Luka Jovic, 21, mwishoni mwa msimu. (Diario Sport)
Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumanne Februari 12, 2019
Reviewed by Zero Degree
on
2/12/2019 07:50:00 AM
Rating: