Loading...

Mashabiki wajiandae kusikiliza kazi yetu mpya - Weusi


WASANII wa kundi la Weusi wameanza kutimiza malengo yao ya kuhakikisha wanaachia kazi baada ya kazi mwaka huu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, mmoja wa wasanii wanaounda kundi hilo, John Makini ‘Joh Makini’, alisema walipanga kuingiza kazi mpya sokoni mapema wiki iliyopita.

Alisema sababu iliyowakwamisha ni msiba wa msanii Godzilla, hivyo tayari muda wowote kuanzia sasa wataachia kazi mpya.

“Tulipisha msiba wa msanii mwenzetu Godzilla, mashabiki wajiandae kusilikia kazi yetu mpya tuliyoshirikiana na wasanii kutoka nchini Kenya,” alisema Joh Makini.

Joh Makini alisema wimbo wao umepewa jina la ‘Kutulia’, huku wakiwa wamewashirikisha Sautisol.
Mashabiki wajiandae kusikiliza kazi yetu mpya - Weusi Mashabiki wajiandae kusikiliza kazi yetu mpya - Weusi Reviewed by Zero Degree on 2/23/2019 03:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.