Loading...

Mwanaharakati aliyepotea Kenya apatikana amefariki


Mwili wa mwanaharakati nchini Kenya Caroline Mwatha umepatikana, msemaji wa polisi Charles Owino ameithibitishia BBC.

Duru zinaarifu kwamba mwili wa marehemu umepatikana katika chumba cha kuhifadhia maiti cha City Mortuary mjini Nairobi.

Caroline Mwatha ni mwanaharakati aliyefanya kazi katika shirika la haki la kijamii katika kitongoji cha Dandora mjini Nairobi, shirika linalonakili visa vya mauaji ya kiholela yaliyotekelezwa na maafisa wa polisi hususan katika vitongoji vinavyoshuhudia uhalifu mkubwa Nairobi.

Caroline inaarifiwa ni mke na mama wa watoto wawili na anatambulika pakubwa kwa machngo wake katika jamii.

Alionekana mwisho Jumatano wiki iliyopita.


Ni mkasa uliozusha mjadala miongoni mwa Wakenya katika mitandao ya kijamii.





Kampeni za kutaka kujua ukweli wa aliko bi Mwatha, ambaye kwa takriban wiki moja leo, alikuwa hajulikani aliko zilianzishwa katika mitandao ya kijamii.

Makundi ya kutetea haki za binaadamu likiwemo Amnesty International na hata mengine kama Missing Voices yalishinikiza kutafutwa kwa Bi Mwatha waliyemtaja kama "mtetezi wa dhati wa haki za binaadamu".

Kwa siku kadhaa familia na marafiki wa marehemu inaarifiwa wamekuwa wakizunguka katika hospitali mbali mbali na hata vyumba vya kuhifadhia maiti wakimtafuta Carolina.


Kwa mujibu wa vyombo vya habari Kenya, Carolina amekuwa akinakili visa vya mauaji yaliotekelezwa na maafisa wa polisi Kenya na visa vya watu kutoweka kiholela.

Baada ya jitihada za wiki nzima, leo uthibitisho umetoka kwamba amefariki.

Duru zinaeleza kwamba alifikishwa katika chumba hicho cha kuhifadhia maiti na mtu binafsi - haijulikani wazi ni lini hasaa alipopelekwa.

Polisi sasa inajaribu kuchambua ni wapi na vipi alipofariki.
Mwanaharakati aliyepotea Kenya apatikana amefariki Mwanaharakati aliyepotea Kenya apatikana amefariki Reviewed by Zero Degree on 2/12/2019 07:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.