Real Madrid yatoa pauni 40m kumnasa straika huyu wa Bundesliga
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 21 anawindwa na klabu ya Barcelona pia lakini Florentino Perez anataka kuwapiku mahasimu wao.
Vilabu vyote viwili vitalazimika kutafuta nguvu mpya katika safu ya ushambuliaji kwenye usajili wa majira ya joto, ikiwa ni kutokana na upungufu wa washambuliaji wa kutosha kukidhi vigezo. Hivi karibuni Barcelona waliagana na Paco Alcacer pamoja na Munir El Haddadi wakati Luis Suarez akitimiza umri wa miaka 32 mwezi uliopita.
Madrid imekuwa kwenye wakati mgumu sana baada ya kuondoka kwa Cristiano Ronaldo. Karim Benzema amefunga mabao 18 kutoa 'assist' 7 katika michezo 37 lakini klabu bado inahitaji kuwa bora zaidi.
Gareth Bale hawezi kuhesabiwa miongoni mwa wachezaji tegemezi kutokana na historia yake ya majeruhi.

Jovic ameonyesha uwezo mkubwa msimu huu, akifunga magoli 14 kwenye michezo 19 ya Bundesliga. Kwa sasa yuko kwenye mkataba wa miaka miwili kutoka Benfica kwa mkopo.
Frankfurt wana kipengele cha kumsajili nyota huyo moja kwa moja kwa pauni milioni 7 katika kipindi cha majira ya joto. Wanaweza kupatanisha dau kubwa baada ya vigogo wa La Liga kuonyesha nia ya kumsajili Jovic.
Frankfurt wana kipengele cha kumsajili nyota huyo moja kwa moja kwa pauni milioni 7 katika kipindi cha majira ya joto. Wanaweza kupatanisha dau kubwa baada ya vigogo wa La Liga kuonyesha nia ya kumsajili Jovic.
Real Madrid yatoa pauni 40m kumnasa straika huyu wa Bundesliga
Reviewed by Zero Degree
on
2/12/2019 07:35:00 PM
Rating: