Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumanne Februari 26, 2019


Manchester United na Chelsea wanamnyatia nahodha wa AC Milan Alessio Romagnoli.

Lakini huenda wakakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa mabingwa wa Serie A, Juventus. (Calciomercato)

Kisa hicho kiliwafanya wachezaji wengi wa Chelsea kumkasirikia kipa huyo wa miaka 24 raia wa Uhispania. (Express)

Leicester City imeongeza juhudi za kumuajiri Brendan Rodgers kutoka Celtic kama meneja wao mpya. (Guardian)

Meneja wa zamani wa Borussia Dortmund Peter Stoger, ambaye amekuwa nje ya kazi tangu alipoondoka Ujerumani mwezi Mei mwaka jana, anapigiwa upatu kuchukua nafasi hiyo kwa mkataba wa kudumu.

Leicester pia inatathmini uwezekano wa kumuajiri meneja wa muda kuchukua nafasi ya Claude Puel hadi mwisho wa msimu huu. (Leicester Mercury)

Mmiliki wa Leeds United Andrea Radrizzani huenda akalazimika kuuza klabu hiyo endapo itashindwa kupanda ngazi ya kushiriki ligi ya primia. (Daily Mail)
Meneja wa Chelsea Maurizio Sarri alimgombeza kipa Kepa Arrizabalaga kwa kupuuza amri yake ya kumtaka kutoka uwanjani wakati wa finali ya kombe la Carabao.

Chelsea inajiandaa kumuuza muingereza Kasey Palmer kwa euro milioni nne, licha ya mchezaji huyo wa miaka 22 kutoshiriki mechi ya wakubwa, huku Bristol City ikitafakari kubadili mkataba wake wa mkopo na kuufanya wa kudumu.

Aaron Wan-Bissaka, 21

Arsenal inaongoza katika kinyang'anyiro cha kumuwania beki wa kulia wa Crystal Palace Aaron Wan-Bissaka,21, na iko tayari kufikia bei ya euro milioni 40 iliyoitishwa na klabu yake. (Sun)

Meneja wa Burnley Sean Dyche, amepuuzilia mbali tetesi kuwa analengwa na Leicester. (Burnley Express)

Nahodha wa zamani wa Manchester United Gary Neville anasema kuwa kutakuwa na ''uasi'' Old Trafford ikiwa klabu hiyo haitamuajiri Ole Gunnar Solksjaer kama meneja wake wa kudumu. (Mirror)

Chanzo: BBC
Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumanne Februari 26, 2019 Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumanne Februari 26, 2019 Reviewed by Zero Degree on 2/26/2019 09:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.