Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumapili Februari 24, 2019


Arsenal inaongoza katika kumwania beki wa kulia wa Crystal Palace Aaron Wan-Bissaka, 21, ambaye anadaiwa kugharimu pauni milioni 40.

Kipa wa klabu ya Burnley na Uingereza Joe Hart, 31, huenda akahamia katika ligi ya MLS. (Sun)

Barcelona iko tayari kutoa dau la pauni milioni 95 kwa kiungo wa kati wa Atletico Madrid Saul Niguez, 24, ambaye pia amehusishwa na uhamisho wa Chelsea. (AS)

Newcastle imeajiandaa kuvunja rekodi yake ya uhamisho na imekubali kumsaini mchezaji wa Brazil Joelinton 22 kwa dau la pauni milioni 51 kutoka Hoffenheim mwisho wa msimu huu. (Sport1)

Manchester United na Bayern Munich wanamfuatilia kiungo wa kati wa Croatia na Barcelona Ivan Rakitic, 30. (Mundo Deportivo)

Mshambualiji Salomon Rondon, 29, ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Newcastle kutoka West Brom, amefichua kuwa anafurahia kusalia katika klabu hiyo hata baada ya mwisho wa msimu huu (Newcastle Chronicle)

Everton imeanza mikakati ya kutaka kumsajili beki wa Paris St-Germain Thomas Meunier, 27. (Le10Sport)

Arsenal inataka kumrudsha winga wake wa zamani Marc Overmars kama mkurugenzi wa kiufundi lakini mpango huo unazuiliwa na klabu yake ya sasa club Ajax.

Arsenal itampatia Rob Holding, 23, mkataba mpya baada ya kupata jeraha la muda mrefu mwezi Disemba. (Mirror)


Beki wa Brazil Marcelo yuko tayari kuondoka Real Madrid na Juventus wanamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30. (Calciomercato)

Muonekano wa Roy Hodgson alipoanza kazi yake ya ukufunzi na muonekano wake wa sasa akiifunza Crystal Palace unampiku Sir Bobby kuwa mkufunzi mzee zaidi katika ligi ya Premia.

Kiungo wa kati wa Barcelona Ivan Rakitic, 30, anasema kuwa anataka kusalia katika klabu hiyo ya Nou Camp baada ya kuulizwa maswali mengi kuhusu kuondoka kwake.. (Marca)

Mkufunzi wa Leicester Claude Puel amewaomba mashabiki wa klabu hiyo kuunga mkono kikosi chake kichanga baada ya kupoteza mechi yao ya nne nyumbani.. (Leicester Mercury)

Mkurugenzi wa klabu ya Liverpool Billy Hogan anasema fedha zitakuwepo kwa mkufunzi Jurgen Klopp mwisho wa msimu huu. (Liverpool Echo)

Chanzo: BBC
Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumapili Februari 24, 2019 Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumapili Februari 24, 2019 Reviewed by Zero Degree on 2/24/2019 07:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.