UEFA: Kuelekea mechi ya United dhidi ya PSG, Draxler amuonya Paul Pogba
Kufuatia kuwasili kwa Ole Gunnar Solskjaer, United wamekuwa na ari Paul Paogba kuwa chachu ya mapinduzi hayo. Kiungo huyo raia wa Ufaransa alikosolewa sana kwa kiwango chake chini ya Jose Mourinho lakini amekuwa kiungo muhimu katika matokeo mazuri ya Mashetani Wekundu.
Ukiachana na kiwangoo kizuri alichoonyesha dhidi ya Fulham, mshindi huyo wa Kombe la Dunia tayari ana magoli 11 msimu huu na ana uhakika wa kuanza na kikosi cha kwanza leo (Jumanne) wakati United itakapocheza dhidi ya PSG kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, UEFA.
Licha ya kukosekana kwa baadhi ya wachezaji tegemezi kikosini Draxler ana amini wachezaji wenzake wanaweza kumdhibiti Pogba.
Kulingana na Sky Sports, Draxler alisema: “Namfahamu Paul muda mrefu sana.
“Nimeshacheza dhidi yake wakati tulipocheza Ujerumani na Ufaransa. Wakati mwingine tulifanikiwa kumdhibiti, tulifanikiwa kumdhibiti nyakati kadhaa.
“Ni mchezaji mkubwa, mwenye sifa za kutosha na aina ya mchezaji ambaye anaweza kufanya makubwa kwenye mechi kubwa za Ligi ya Mabingwa.
“Lakini tuna wachezaji wazuri, ambao nafikiri wana uwezo wa kumdhibiti.”
UEFA: Kuelekea mechi ya United dhidi ya PSG, Draxler amuonya Paul Pogba
Reviewed by Zero Degree
on
2/12/2019 03:35:00 PM
Rating: