Wadau wanazungumza nini kuhusu uamuzi wa Aaron Ramsey
Ukizingatia mikataba aliyopewa, Arsenal haingeliweza kuendelea kumlipa sawa na wachezaji wake wengine.
Nakumbuka Arsene Wenger alisema matukio kama hayo yatakua ya kawaida.
Wachezaji wanapewa ofa kubwa kiasi cha wao kuthubuti kuvunja mikataba waliyo nayo.
Katika umri huu, thamani yake ni angalau pauni milioni 30-40. Juventus wanaweka akiba ya fedha nyingi hata baada ya kumlipa kitita hicho kikubwa.
Ni hatua ambayo mtu yoyote hatachelea kuchukua isipokuwa klabu anayotoka.
Mshambuliaji wa zamani Blackburn Chris Sutton:
Arsenal wamefanya makosa kuwaachia wachezaji mwanya wa kutengua mikataba yao.
Zama zetu, unapewa mkata mwingine ukisalia na miaka miwili kabla ya mkataba wako kukamilika, ikiwa klabu inathamini mchango wako.
Arsenal wamejipalia wenyewe makaa ya moto.
Wadau wanazungumza nini kuhusu uamuzi wa Aaron Ramsey
Reviewed by Zero Degree
on
2/12/2019 01:20:00 PM
Rating: