Loading...

Baba wa Thibaut Courtois avishutumu vyombo vya habari kwa kumnyanyasa mwanaye


Baba mzazi wa golikipa wa Real Madrid Thibaut Courtois amevishutumu vyombo vya habari vya Uhispania kwa kumnyanyasha mwanaye.

Golikipa huyo wa timu ya taifa ya Ubelgiji amekuwa akikosolewa mara kadhaa na vyombo vya habari kufuatia klabu hiyo kupoteza mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Ajax.

Baba wa nyota huyo amesistiza kwamba vyombo vya habari mjini Madrid vimekuwa vikimzungumzia vibaya mwanaye baada ya mechi ya vigogo hao wa La Liga dhidi ya Ajax kwenye Ligi ya Mabingwa. Mbelgiji huyo aliruhusu magoli manne katika usiku mmoja na kuwafanya mabingwa hao wa Ligi ya Mabingwa kutolewa katika hatua ya 16 bora katika hali ya kushangaza wakiwa kwenye uwanja wao wa Santiago Bernabeu licha ya kuondoka na ushindi wa bao 2-1 ugenini. Mshindi wa tuzo ya golikipa bora wa dunia mwaka 2018 alisajiliwa na vigogo hao kwenye majirra ya joto akitokea Chelsea.



Kwa mujibu wa taarifa ya DailyMail, Baba wa Courtois alisema, “Nafikiri kwamba kila mtu anamlenga Thibaut. Vyombo vya habari wa Uhispania, na pia Ubelgiji. Mimi kama baba, siwezi kulikalia kimya jambo hili.”

Aliongeza, “Siku zote golikipa anakuwa wa kwanza kulaumiwa, ni sehemu ya kazi. Iwe kwa usahihi au makosa, siwezi kuwaachia mtoe hukumu. Lakini baada ya mchezo dhidi ya Ajax, alilengwa yeye pekee kwa sababu ya bao la nne baada ya kuwa amecheza vizuri. Hili kosa moja pekee limezua makubwa. Kuna vitu binafsi pia vinatajwa na vyombo vya habari. Ninayaona malengo ya waandishi wa habari kwa mwanangu. Nalipigania hilo, lakini kwa bahati nzuri mwanangu ni zaidi ya hayo. Anajua nini cha kufanya na anaelewa uwezo wake na kamwe hatajihofia.”
Baba wa Thibaut Courtois avishutumu vyombo vya habari kwa kumnyanyasa mwanaye Baba wa Thibaut Courtois avishutumu vyombo vya habari kwa kumnyanyasa mwanaye Reviewed by Zero Degree on 3/13/2019 09:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.