Loading...

Ephraim Kibonde azikwa makaburi ya Kinondoni


Aliyekuwa Mtangazaji wa Clouds Media Group (CMG), Ephraim Kibonde amezikwa leo Machi 10 katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es salaam majira ya saa Kumi jioni.

Amezikwa na maelfu ya watu ambao ni ndugu, jamaa na marafiki aliokuwa akifanya nao shughuli mbalimbali enzi za uhai wake na wengine waliomjua kupitia kazi yake ya utangazaji.

Kibonde alifariki dunia Machi 7 mwaka huu baada ya kuugua Presha kwa muda mfupi akiwa kwenye mazishi ya Ruge Mutahaba.

Ameacha watoto watatu, wakike wawili na mmoja wakiume.
Ephraim Kibonde azikwa makaburi ya Kinondoni Ephraim Kibonde azikwa makaburi ya Kinondoni Reviewed by Zero Degree on 3/09/2019 05:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.