Loading...

CAF: Simba yakubali kichapo cha bao 2-0


MCHEZO wa Ligi ya hatua ya makundi kati ya JS Saoura na Simba ya Tanzania ngoma imekuwa ngumu kwa wawakilishi kutoka Tanzania ambapo wamekubali kichapo cha mabao 2-0.

Katika mchezo wa leo Simba walikuwa wamepoteana tangu kipindi cha kwanza ambapo kila mchezaji alicheza kama yupo Ligi Kuu Bara hali iliyowapa nafasi wapinzani wao JS Saoura kuwashambulia na kupata bao la kwanza dakika ya 18 ambalo lilidumu mpaka mapumziko.

Kipindi cha pili wachezaji wa Simba walionekana kujisahau tena na kuendelea kuutafuta mpira kama ni mchezo wa kirafiki huku wakishindwa kumiliki mpira.

Bao la pili la JS Saoura lilifungwa dakika ya 51 na kufanya matokeo kuwa 2-0 .

Matokeo hayo yanaipa wakati mgumu Simba kufuzu hatua ya robo fainali kutokana na milango kuwa migumu hasa kundi D ambalo kocha wa Simba Patrick Aussems alisema lipo wazi.
CAF: Simba yakubali kichapo cha bao 2-0 CAF: Simba yakubali kichapo cha bao 2-0 Reviewed by Zero Degree on 3/09/2019 11:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.