Mbowe asikitishwa Lowassa kuondoka Chadema
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Ijumaa Machi 15, Mbowe amesema walimpokea Lowassa mwaka 2015 kwa nia njema lakini leo kaamua kurudi CCM.
“Kwenda kwenye chama kingine cha siasa siyo mbaya, basi akaseme kweli na akisaidie chama hicho kisiendelee kuwatesa Watanzania na sisi tutaendelea kuijenga demokrasia.
“Enzi za uhai wake Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, aliwahi kusema chama cha siasa ni dodoki ukiliweka kwenye maji litanyonya maji na ukiliweka kwenye maziwa litanyonya maziwa kilichobaki ni kujenga chama kwa kuongeza wanachama,” amesema Mbowe.
Chanzo: Mtanzania
Mbowe asikitishwa Lowassa kuondoka Chadema
Reviewed by Zero Degree
on
3/15/2019 03:50:00 PM
Rating:
Reviewed by Zero Degree
on
3/15/2019 03:50:00 PM
Rating:
