Loading...

Messi aukubali muziki wa Ronaldo


STRAIKA Lionel Messi, amempigia saluti mwenzake, Cristiano Ronaldo, kwa jitihada alizozifanya juzi ikiwa ni baada ya yeye kuonesha kiwango kizuri kilichoisaidia Barcelona kuichapa Lyon katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora.

Katika mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Nou Camp, Messi alifunga mabao mawili na kutengeneza mengine mawili yaliyoifanya Barca kuondoka na ushindi wa mabao 5-1, zikiwa ni wiki tatu baada ya mchezo wa kwanza timu hizo kushindwa kutambiana.

Ushindi huo ulikuja ikiwa ni baada ya juzi hasimu wake, Ronaldo kutupia ‘hat-trick’ iliyoisaidia Juventus kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Atletico Madrid na hivyo kutinga robo fainali kwa jumla ya mabao 3-2.

Kufuatia hali hiyo, Messi, alikaririwa na gazeti la Marca baada ya mchezo huo na Lyon akisema: “Kile ambacho Cristiano Ronaldo na Juventus walikifanya ni cha kuvutia.

“Nafikiri Atletico Madrid ilikuwa ni timu ngumu, lakini Ronaldo alikuwa na usiku wa maajabu kwa kufunga mabao matatu.”
Messi aukubali muziki wa Ronaldo Messi aukubali muziki wa Ronaldo Reviewed by Zero Degree on 3/15/2019 02:20:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.