Loading...

Mtambo wa kuchakata asali wafungwa Manyoni

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS)Profesa Dos Sontos Silayo na Kulia ni Meneja wa Wilaya ya Manyoni TFS Juma Mchafu.

WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania( TFS) imefunga mtambo wa kuchakata mazao ya nyuki wilayani Manyoni mkoani Singida wenye uwezo wa kuchakata asali lita 500 kwa siku.

Mtambo huo uliogharimu Sh80 milioni unatarajiwa kuondoa tatizo la ubora duni wa asali na nta katika ukanda huo na maeneo ya jirani.

Taarifa ya Mkuu wa Kitengo cha Mawasilino wa TFS, Tulizo Kilaga amesema leo kuwa mtambo huo umefungwa katika kiwanda cha lakini pia wafugaji wa nje wataruhusiwa kuchakata mazao yao.

Amesema kiwanda hiko kwa kiasi kikubwa kitategemea mali ghafi toka kwenye misitu Aghondi uliopo eneo la Itigi. Amefafanua kwamba katika uvunaji wa awali wamefanikiwa kuvuna mizinga 459 kati ya 729 na kupata asali kilo 6,175 sawa na tani 6.175 wastani kilo 13.45 kwa mzinga.
Mtambo wa kuchakata asali wafungwa Manyoni Mtambo wa kuchakata asali wafungwa Manyoni Reviewed by Zero Degree on 3/14/2019 01:01:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.