Loading...

Rais Felix Tshisekedi amewaachilia huru mamia ya wafungwa wa kisiasa

Wakati wa kuapishwa kwake, rais Felix Tchisekedi aliahidi kuwaachilia wafungwa wa kisiasa


Hatua ya Rais Felix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuwaachilia huru wafungwa 700 wa kisiasa imeendelea kuzua mjadala kote nchini humo.

Mashirika ya kutetea haki za binadamu yamempongeza rais Tshisekedi kwa kutimiza ahadi yake na kuwaachilia huru wafungwa hao.

''Kuna matumaini makubwa katika utawala huu hasa katika suala la kuheshimu haki za binadamu'', mmoja wa wanaharakati aliiambia BBC.

Kwa mujibu wa idara magereza nchini DRC wafungwa hao wanasubiri barua rasmi ya serikali kabla ya kuruhusiwa kutoka gerezani.

''Huu ni mchakato ambao unaweza kuchukuwa siku moja au zaidi, sidhani kama leo wataachiliwa huru na kurejea makwao'', Mmoja wa maafisa wa magereza ambaye hakutaja jina lake litajwe aliiambia BBC.

Mkurugenzi wa baraza la mawaziri, Vital Kamerhe, alitangaza hatua hiyo ya rais kwa taifa usiku wa Jumatano.

Miongoni mwa wafungwa waliyoachiliwa huru ni Firmin Yangambi, wakili aliyekamatwa mwaka 2009 na kuhukumiwa kifo mwaka mmoja baadae.

Wakili huyo alituhumiwa kwa kumiliki silaha kinyume cha sheria na jaribio la kupanga maandamano dhidi ya serikali.

Mwingine ni Franck Diongo ambaye alikamatwa mwaka 2016 kwa tuhuma za kuzuilia mali ya walinzi watatu wa rais kwa kutumia amri ya mahakama.

Bwana Kamerhe pia alisema kuwa watu wote waliyokamatwa kwa kushiriki maandamano ya kupigania demokrasia kati ya mwaka 2015 na 2018 wataachiliwa huru.

Hatua ilipaswa kuchukuliwa mwaka 2015 kama sehemu ya mwafaka wa kisiasa uliyofikiwa chini ya usimamizi wa kanisa katoliki uliyopendekeza wafungwa wote wa kisiasa kuachiliwa huru kabla ya kuandaliwa kwa uchaguzi.

Katika mwafaka huo kanisa katoliki pia lilipendekeza wanasiasa wa nchi hiyo wanaoishi uhamishoni waruhusiwe kurudi nyumbani.

Hatua hiyo imepokelewaje?

Kando na kuachiliwa kwa wafingwa hao mashirika ya kutetea haki za binadamu pia yamepongeza hatua ya kusimamishwa kazi kwa maafisa wa ngazi ya juu serikalini ambao wanatuhumiwa kwa visa vya ulaji rushwa.

Wananchi wa DRC walitumia mitandao wa kuelezea furaha yao huku wengine wakisema kuwa sasa viongozi wafisadi wataogopa kuchukuliwa hatua na serikali.

Baadhi yao waliyosimamishwa kazi ni wandani wa karibu wa rais wa zamani Joseph Kabila.

''Hii inaonesha wazi kuwa rais Tshisekedi anafanya maamuzi yake mwenyewe haongozwi na Kabila'' alisema mmoja katika mtandao wa kijamii wa Twitter.Mashirika ya kutetea haki za binadamu yalihoji kukamatwa na kuzuiliwa kwao yakidai kuwa yalichochewa kisiasa.

Rais felix Tchisekedi (kulia) akiwa pamoja na mtangulizi wake Joseph kabila


Wakati wa kuapishwa kwake Rais mpya wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Felix Tshisekedi, aliahidi kuwaachilia huru wafungwa wote wa kisiasa wakiwemo watu wote waliofungwa wakati wa maandamano yaliyofanyika kabla ya uchaguzi wa mkuu wa mwezi wa Disemba mwaka jana.

Bwana Tshisekedi alikuwa mgombea wa upinzani katika uchaguzi uliibua mgawanyiko na shutuma kwamba kulikuwa na wizi wa kura ili kuwazuwia wakosoaji wa rais Joseph Kabila kuingia madarakani.

Katika hotuba yake aliyoitoa katika mji mkuu wa nchi hiyo Kinshasa rais wa Kongo , Felix Tshisekedi, amesema ''Nitamuomba waziri wa sheria kuwa kuwaachilia huru wafungwa wote wa kisiasa waliowekwa gerezani kwa ajili ya maoni yao''.

Bwana Tshisekedi aligombea kama kiongozi wa upinzani katika uchaguzi uliokuwa na utata wa Disemba mwaka jana baada ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo Joseph Kabila kung'atuka madarakani.

Hata hivyo Mahakama ya katiba DR Congo ndiyo iliyomuidhinisha rasmi Felix Tshisekedi kuwa rais wa nchi hiyo, na ilikataa ombi la rufaa iliowasilishwa na Martin Fayulu.
Rais Felix Tshisekedi amewaachilia huru mamia ya wafungwa wa kisiasa Rais Felix Tshisekedi amewaachilia huru mamia ya wafungwa wa kisiasa Reviewed by Zero Degree on 3/14/2019 01:00:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.