Loading...

Neymar hatarini kuadhibiwa kufuatia kauli yake baada ya PSG kuondolewa UEFA


Neymar anatarajia kuchunguzwa na UEFA baada ya kutoa lugha chafu kwenye mitandao ya kijamii kufuatia Paris Saint Germain kufungwa mabao 3-1 dhidi ya Manchester United kwenye Ligi ya Mabingwa.

Mabingwa hao wa ligi kuu ya Ufaransa walitolewa kwenye michuano hiyo ya Ulaya dakika za mwisho kwa mkwaju wa penalti uliopatikana baada ya tekinolojia ya VAR kuhusika. Mpira uliopigwa na Diogo Dalot ulienda kugonga mkono wa Presnel Kimpembe na awali mwamuzi akashindwa kuligundua hilo.

Mwamuzi Damir Skomina alilazimika kutumia tekinolojia ya VAR pamoja na kutazama marudio kwenye TV kabla ya kutoa uamuzi. Marcus Rashford aliitumia nafasi hiyo kuvusha timu yake hadi hatua ya robo fainali na kuwaacha Wafaransa hao midomo wazi katika dakika za mwisho.

Neymar akiwa jukwaani wakati wa mchezo kati ya Paris Saint-Germain na Manchester United
Neymar ambaye anauguza majeraha ya mguu alikuwa anaushuhudia mchezo huo akiwa nje na baada ya mchezo huo kuisha aliekeza hasira yake kwenye mitandao ya kijamii. “Hii ni dharau kabisa, wanaweka watu wanne ambao hawajui chochote kuhusu mpira wa miguu kusimamia marudio ya kwenye VAR.

“Hakuna penalti. Unasema amecheza kwa mkono wakati mpira umegonga mgogoni! Nendeni ....huko!”

UEFA walitoa kauli hii: “Kwa mujibu wa kifungu namba 31 (3) (a) cha taratibu za kinidhamu za UEFA, UEFA leo imetangaza kwamba imemteua mchunguzi wa masula ya maadili na nidhamu kufanya uchunguzi wa maoni yaliyotolewa na mchezaji wa Paris Saint-Germain Neymar kwenye mitandao ya kijamii, kufuatia mchezo wa Ligi ya Mabingwa msimu wa 2018/19 kati ya Paris Saint-Germain na Manchester United, uliochezwa Machi 6, 2019 nchini Ufaransa.”
Neymar hatarini kuadhibiwa kufuatia kauli yake baada ya PSG kuondolewa UEFA Neymar hatarini kuadhibiwa kufuatia kauli yake baada ya PSG kuondolewa UEFA Reviewed by Zero Degree on 3/14/2019 11:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.