Nedved amkingia kifua Ronaldo, ni kuhusu staili yake ya kushangilia
Mreno huyo aliondoka Santiago Bernabeu kwenye majira ya joto mwaka jana kwenda Juventus.
Mkurugenzi wa michezo wa Juventus na nyota wa zamani wa klabu hiyo Pavel Nedved amesistiza kwamba nyota huyo wa Ureno Cristiano Ronaldo aliukanawa Atletico Madrid katika mchezo wao wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa. Vigogo hao wa Uhispania waliibuka kidedea katika mchezo huo kwa ushindi wa mabao 2-0. Hata hivyo, maajabu yaliofanywa na Ronaldo, ambaye alifunga hat-trick dhidi ya Atletico, yaliwawezesha wakongwe hao wa Italia kupindua meza na kuibuka kidedea kwa ushindi wa mabao 3-0 na kufuzu kwa hatua inayofuata.
Hata hivyo, moja ya vitu vinavyozunguziwa kwa sana ni namna Mreno huyo alivyoshangilia baada ya kupachika bao la pili kufanya mzaha kwa namna ya ushangiliaji iliyotumiwa na meneja wa Atletico Madrid Diego Simeone katika mchezo wa kwanza baada ya timu yake kuibuka na ushindi. Kumekuwa na uvumi kuwa UEFA wanaweza kumfungia Ronaldo kufuatia namna hiyo ya ushangiliaji na Nedved ameamua kuvunja ukimya juu ya suala hilo.
Kwa mujibu wa taarifa ya Sky Sports Italia, mkongwe huyo alisema, “Sihofii adhabu yoyote. Ni ishara ambayo inatakiwa kubaki uwanjani. Hisia zinazoonyeshwa uwanjani zinatakiwa kubaki pale.”

Reviewed by Zero Degree
on
3/16/2019 09:35:00 AM
Rating: