Loading...

RASMI: Real Madrid wakamilisha usajili wa Eder Militao



Real Madrid wametangaza kumsajli beki wa kati wa klabu ya FC Porto Eder Militao. Militao tayari ameshasaini mkataba wa miaka 6 na vigogo hao wa La Liga na atajiunga nao msimu ujao. Militao alijiunga na Porto akitokea Sao Paulo kwenye majira ya joto na ameonyesha uwezo mkubwa akiwa na klabu hiyo msimu huu.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 21 ameshiriki katika michezo 34 akiwa na Porto msimu huu, akifunga mabao matatu na kutoa 'assist' mbili. Msimu huu, Militao ametajwa kuwa beki bora wa mwezi kwenye Ligi Kuu ya Ureno katika matukio 5 tofauti. Militao alitwaa tuzo hiyo kwa miezi ya Septemba, Octoba, Novemba, Decemba na Januari.

Amekuwa sehemu muhimu kwa Porto katika harakati za kushangaza hadi kufuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa. Vilabu kadhaa vilionyesha nia ya kutaka kumsajili Militao. Ikiwa ni pamoja na Manchester United na Liverpool. Hata hivyo, Real Madrid walionekana kuwa mbele zaidi siku zote na hadi kufanikiwa kumsajili.

Eder Militao, 21

Militao pia ameshashiriki katika mchezo mmoja wa kimataifa akiwa na timu ya taifa ya Brazil. Mchezo wake wa kwanza ulikuwa ni ule wa kirafiki kati ya Brazil na El Salvador mwezi Septemba mwaka jana. Militao pia ni miongoni mwa wachezaji walioitwa kuunda kikosi cha timu ya taifa ya Brazil kitakachocheza mechi za kirafiki dhidi ya Panama na Jamhuri ya Czech.

Eder Militao atakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na Real Madrid chini ya uongozi wa Zinedine Zidane. Mbrazil huyo atakuwa na wakati mgumu kuhakikisha ana pata nafasi atakapotua Real Madrid kwa sababu atakuwa anashindania namba na wakongwe kama Sergio Ramos na Raphael Varane kwenye kikosi cha kwanza.
RASMI: Real Madrid wakamilisha usajili wa Eder Militao RASMI: Real Madrid wakamilisha usajili wa Eder Militao Reviewed by Zero Degree on 3/14/2019 10:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.