Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya leo Ijumaa Machi 8, 2019


Meneja wa zamani wa Manchester United Jose Mourinho yuko tayari kurejea Real Madrid hadi mwishoni mwa msimu huu.

Liverpool itaangalia namna ya kupata mkopo utakaowasaidia kumchukua mchezaji wa Ligi ya Primia Harry Wilson msimu ujao - lakini kuwasili kwa Brendan Rodgers katika Leicester kunaweza kumaliza matumaini ya Foxes ya kusaini mkataba na winga huyo mwenye umri wa miaka 21, ambaye kwa sasa anacheza kwa deni katika Derby. (Goal)

Meneja wa zamani wa Chelsea, Leicester na Fulham Claudio Ranieri, mwenye umri wa miaka 67, anakaribia kukamilisha taratibu za kuichukua klabu yake ya zamani Roma, a baada ya upande wa ligi hiyo ya dataja la A kumfuta kazi Eusebio di Francesco. (Sky Sports)

Manchester United wanaangalia uwezekano wa kumtoa kwa timu nyingine winga wao Mjerumani mwenye umri wa miaka 19 kwa deni -kwa msimu wote ujao.

Meneja wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane, mwenye umri w amiaka 46, ambaye amehusishwa na Chelsea, anasakwa na klabu ya Uhispania na pia Juventus. (Sun)


Tottenham wamo katika harakati za kurejea White Hart Lane na Haringey Council huku wakitoa taarifa kwa maafisa wa usalama barabarani wakiwataka wahakikishe usalama wa barabarani kwa ajili ya majaribio ya matukio kuanzia mwishoni mwa juma lijalo

Meneja wa Juventus Massimiliano Allegri, mwenye umri wa miaka 51, amefichua kuwa mazungumzo kuhusu hatma yake ya siku zijazo yamesitishwa hadi mwishoni mwa msimu. (Mail)

Mshambuliaji wa Real Madrid Mhispania Isco, akiwa na umri wa miaka 26, ''amemkasirikia'' meneja wake Santiago Solari na ameelezea nia yake ya kuwasiliana na Manchester City. (Calciomercato)

Nahodha wa Real Madrid na Uhispania Sergio Ramos alikuwa na malumbano makali na rais wa klabu hiyo Florentino Perez kufuatia klabu hiyo kufungwa dhidi ya Ajax, huku Perez akitishia kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32. (Marca)

Meneja wa England Gareth Southgate anasisitiza kuwa hakuna mtizamo hasi dhidi ya wachezaji wanaochezea katika mataifa ya kigeni kama winga Jadon Sancho mwenye umri wa miaka 18- alivyofanya kwa timu ya Ujerumani ya Borussia Dortmund. (Talksport)

Liverpool na Everton wmekuwa wakihusishwa na mchezaji wa safu ya mashambulizi wa Real Sociedad ya Uhispania Diego Llorente, mwenye umri wa miaka 25. (Liverpool Echo)

Mawakala wa Uingereza wamejipanga kukabiliana na Fifa baada ya taarifa juu ya sheria mpya ambazo zinatoza faini zake moja kwa moja na kwa mchezaji wanayemuwakilisha. (Telegraph)

Pablo Sarabia

Mchezaji wa safu ya kati wa Sevilla Muhispania Pablo Sarabia, mwenye umri wa miaka 26, amekataa kuhamia Chelsea mwezi Januari ambacho ndio kipindi cha mwisho cha wachezaji kuhama. (Mundo Deportivo)

Mmiliki wa klabu ya Lille Gerard Lopez amefichua kwamba itagharibu walau pauni milioni £43m kumtoa winga Nicolas Pepe, mwenye umri wa miaka 23 raia wa Ivory Coast huku pia akikanusha mkuruhgenzi wa michezo wa Louis Campos anafanya mazungumzo na Chelsea. (RMC Sport)

Mchezaji wa safu ya mashambulizi katika mbwa mwitu(wolves) Leo Bonatini, mwenye umri wa miaka 24, ambaye anacheza kwa deni katika timu ya Nottingham Forest kwa muda uliosalia wa msimu, anataka kubakia City Ground kwa muhula ujao - Forest wapande daraja wasipande . (Express & Star)

Charlton wamepokea maombi mapya ya thamani ya pauni milioni £30m, kutoka kwa afisa wa zamani wa benki mwenye uzoefu wa kiwango cha juu cha soka. 

Mchezaji wa Tottenham, na Uimgereza anayecheza Dele Alli, 22 ana matumaini ya kurejea baada ya kupata majeraha wikendi. (London Evening Standard)

Mshambuliaji klabu ya Uingereza ya Leicester Jamie Vardy, mwenye umri wa miaka 32, atakua fiti kwa ajili ya kukabiliana na Fulham Jumamosi hii baada ya kufanyiwa upasuaji wa kushona ulimi wake kufuatia kugongana kwake na na Ben Foster ambapo walishindwa 2-1 katika uwanja wa Watford wikendi iliyopita

Brendan Rodgers amepuuza tetesi kwamba afisa mkuu wa kitengo cha utoaji wa kazi wa Celtic Lee Congerton atajiunga nae katika Leicester. (Leicester Mercury)

Mchezaji wa safu ya ulinzi wa timu ya Brighton Inigo Calderon, mwenye umri wa miaka 37, amerejea katika klabu ya nyumbani Alaves, nchini Uhispania kama kocha msaidizi kwenye timu hiyo iliyopo kwenye daraja la B nadi mwishoni mwa msimu. (Argus)

Chanzo: BBC
Tetesi za soka barani Ulaya leo Ijumaa Machi 8, 2019 Tetesi za soka barani Ulaya leo Ijumaa Machi 8, 2019 Reviewed by Zero Degree on 3/08/2019 08:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.