Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumamosi Machi 16, 2019


Real Madrid wanalenga kumsajili Raheem Sterling kama sehemu ya mipango yao ya kurejesha makali ya kikosi chao, huku meneja wa klabu hiyo Zinedine Zidane akiwa shabiki mkubwa wa Mwingereza huyo.

Kiungo wa klabu ya Wolves, Joao Moutinho ameeleza kuwa alikaribia kujiunga na Everton pamoja na Tottenham kabla ya kwenda Molineux.

Mlinda mlango wa Newcastle Martin Dubravka anaweza kuondoka katika klabu hiyo kama hataongezwa mshahara, kwa mujibu wa wakala wake. (Mirror)

Eden Hazard anaweza kuipotezea Real Madrid na kuamua kusalia katika klabu ya Chelsea.

Luis Suarez amedai kuwa Steven Gerard alikuwa miongoni mwa watu waliomshawishi aipotezee Arsenal akajiunge na Barcelona.

Klopp anasema kuwa mstakabali wake utaamliwa na mwenyezi Mungu, na sio kwa mataji atakayotwaa akiwa na Liverpool. (talkSport)

Manchester City wanataka kumwajili kiungo wa klabu ya Roma Daniele De Rossi kama mkufunzi wa shule yao atakapostafu soka kama mchezaji.

Wachezaji wa Fulham walibaki katika hali ya mkanganyiko kwa mfumo wa Claudio Ranieri kuwafanya wafanye mazoezi ya mpira wa mikono siku moja kabla ya mechi.

Olivier Giroud ameonyesha nia ya kutaka kuondoka Chelsea baada ya kueleza kuwa hataendelea kuitumikia klabu hiyo kama mchezaji wa akiba.

Arsenal walijaribu kuishawishi Rennes kumuuza nyota wao Ismaila Sarr mara tu baada ya kufungwa mabao 3-1 nchini Ufaransa wiki iliyopita.

Kylian Mbappe na Adrien Rabiot kwa pamoja wote walipigwa faini ya pauni 150,000 kwa kosa la kuchelewa kwenye mkutano wa klabu ya Paris Saint-Germain. (Sun)

Manchester City wanatarajiwa kupewa adhabu ile ile na Fifa, kufungiwa kufanya usajili kama Chelsea kwa kukiuka taratibu za usajili wa wachezaji wenye umri mdogo. (Times)

Steven Gerrard amekubali kuwa anaweza kufukuzwa kazi Rangers kama hataweza kuweka mikakati ya usajili yenye tija na kama atashindwa kuipatia klabu hiyo kikombe chochote msimu ujao.

Chris Brunt ana matamanio makubwa ya kubaki katika klabu ya West Brom lakini anakubali kuwa wachezaji wengi watauzwa kama klabu hiyo haitafanikiwa kupanda daraja msimu huu. (Express)

Andreas Christensen

Chelsea watakwepa adhabu kwa kufanya malipo kwa baba mzazi wa Andreas Christensen kinyume na taratibu mwaka 2015. (Daily Mail)

Meneja wa timu ya taifa ya Uingereza Gareth Southgate anatarajiwa kumwita James Ward-Prowse kikosini kufuatia Jordan Henderson kuumia katika mechi ya Ligi ya Mabingwa kati ya Liverpool na Bayern Munich. (Telegraph)

Pep Guardiola amaitaka timu ya taifa ya Uingereza kumruhusu John Stones asifike kazini, akidai kuwa beki huyo wa Manchester City hayuko 'fiti' kwa michezo ya kufuzu kushiriki michuano ya Euro 2020 dhidi ya Jamhuri ya Czech na Montenegro.

Nyota wa Crystal Palace Wilfried Zaha yuko hatarini kuukosa mchezo wa FA dhidi ya Watford wikendi hii baada ya kuumia mazoezini. (Guardian)
Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumamosi Machi 16, 2019 Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumamosi Machi 16, 2019 Reviewed by Zero Degree on 3/16/2019 07:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.