Loading...

Wanafunzi wa madarasa 3 wasoma kwa zamu


SHULE ya Msingi Diovuva iliyopo katika Kata ya Kiroka Halmashauri Wilaya ya Morogoro inakabiliwa na ya uhaba wa madarasa, hali inayowalazimu wanafunzi wa madarasa matatu kusoma kwa zamu.

Kwa mujibu wa taarifa ya HabariLeo, Mkuu wa Shule Msaidizi, Honorius Ngachipanga alisema ujenzi wa madarasa hayo uko chini ya serikali ya kijiji. Ngachipanga alisema shule hiyo ina wanafunzi 682 ambapo wavulana 360 na wasichana 322.

Alisema kuwa shule hiyo kwa sasa ina madarasa saba wakati mahitaji ni 15. Aidha hali hiyo inasababisha baadhi ya wanafunzi hasa wa darasa la kwanza, chekechea na darasa la pili kusoma kwa zamu katika darasa moja.

“Wakati wa mvua tunalazimika kuwaweka wanafunzi wa madarasa yote matatu kwa pamoja na walimu wao kisha wanafundishwa kwa zamu wakiwa wote humohumo,” alisema. Alisema kuwa hali hiyo imekuwa ni changamoto kubwa kwa walimu na wanafunzi hao ambapo alisema kuwa wakati mwingine wakifundishwa wa darasa moja wengine wanaendelea kupiga kelele, jambo ambalo alisema kuwa ni usumbufu kwa wengine.

Aidha aliitaja changamoto nyingine kuwa ni uhaba wa matundu ya vyoo. Mahitaji ni 28 wakati matundu yaliyopo ni 12 na kwamba wanakabiliwa na changamoto ya nyumba za walimu ambapo alisema walimu walimu wengi wanaishi nje ya shule.

Ngachipanga alisema pia wanakabiliwa na changamoto ya watoto wa kike kuanza mahusiano ya kingono wakiwa bado wadogo hali inayowafanya baadhi yao kushindwa kuendelea na masomo.

Alisema kwa wanafunzi wa darasa la saba wa mwaka huu, tayari mmoja ameshaacha masomo kwa kupata ujauzito. Alisema kuwa matatizo mengine yanachangiwa na wazazi ambao wengine wamekuwa wakiwapeleka watoto kujiunga na njia za uzazi wa mpango wakiwa bado wadogo. Kwa upande wake Ofisa Elimu Kata ya Kiroka, Peter Mwanja alisema wameihamasisha jamii kuhakikisha inajitoa kwa ajili kuchangia nguvu kazi
Wanafunzi wa madarasa 3 wasoma kwa zamu Wanafunzi wa madarasa 3 wasoma kwa zamu Reviewed by Zero Degree on 3/02/2019 02:20:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.