Mazungumzo ya muafaka wa Brexit Uingereza yavunjika
Chama cha upinzani cha Labour nchini Uingereza kimevunja mazungumzo ya wiki sita sasa ya Brexit ya kupata muafaka na waziri mkuu Theresa May,na kulalamika kuwa mamlaka yake yanayeyuka na utawala wake unakaribia mwisho.
Kiongozi wa chama cha labour Jeremy Corbyn amesema mpasuko kati yao hauwezi kuzibwa, na ile hali ya kujiamini haipo tena kwamba mrithi wake ataendelea na maridhiano yoyote yanayoweza kupatikana. Majadilino "yamekwenda hadi yalipofikia," Corbyn amesema katika barua kwa May.
"Ongezeko la udhaifu na kutokuwa thabiti kwa serikali yako kuna maana hakutakuwa na imani katika kulinda chochote kinachoweza kukubaliwa baina yetu," amesema.
Corbyn amesema chama cha Labour kwa hiyo kitaendelea kupinga makubaliano ya taalka yaliyofikiwa na serikali kama yalivyo hivi sasa.
Wabunge mara tatu waliyakataa makubaliano yaliyofikiwa na May pamoja na Umoja wa Ulaya, na kumlazimisha kuchelewesha tarehe ya Brexit mara mbili na kukinyooshea mkono chama cha Labour.

Bunge linatarajiwa kupiga kura kwa mara ya nne mapema mwezi Juni kuhusiana na masharti ya Uingereza kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya.
May ambaye ameonekana kuchoka alisema wabunge watakabiliwa na kile alichosema kuwa ni " chaguo gumu": kupiga kura kukubaliana na Brexit , ama "kukataa tena".
Alikuwa akizungumza katika tukio mahsusi la kampeni kabla ya uchaguzi wa bunge la Ulaya, utakaofanyika nchini Uingereza siku ya Alhamis, ambapo maoni ya wapiga kura yanaonesha chama chake cha Conservative kinaweza kushika nafasi ya tano.
Uingereza haikutaka kushiriki katika uchaguzi huo lakini itafanya hivyo kwasababu ya kuahirishwa kwa Brexit.

Bango linalosisitiza Uingereza kubakia katika Umoja wa Ulaya wakati wa maandamano mjini London |
Kuvunjika kwa mazungumzo hayo kumekuja siku moja baada ya May kukubali kuweka muda maalum kwa ajili ya kuachia wadhifa wa uwaziri mkuu kufuatia kura ya kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya bungeni, ambayo itafanyika katika muda wa wiki moja kuanzia Juni 3. Makubaliano hayo yamefikiwa katika mkutano wa faragha pamoja na wanachama na viongozi wa wabunge wa chama cha Conservative.
Inafikiriwa kwamba May atazindua mpambano wa kuwania nafasi ya uongozi mara mswada wa makubaliano ya kujitoa ama ukishindwa, kama inavyoonekana kuwa , ama utakamilishwa.
Inafikiriwa kwamba May atazindua mpambano wa kuwania nafasi ya uongozi mara mswada wa makubaliano ya kujitoa ama ukishindwa, kama inavyoonekana kuwa , ama utakamilishwa.
Mazungumzo ya muafaka wa Brexit Uingereza yavunjika
Reviewed by Zero Degree
on
5/17/2019 04:05:00 PM
Rating: