Loading...

Ngassa aondolewa kambini Yanga


KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa juzi alfajiri aliondolewa kambini baada ya kuugua malaria ghafla. Ngassa aliondolewa kwenye kambi hiyo ikiwa ni saa chache kabla ya timu hiyo kuingia kambini Nefaland Hotel iliyopo Manzese jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa gazeti la Championi, Ngassa alisema kuwa hatakuwepo sehemu ya kikosi kilichoivaa Ruvu Shooting jana saa kumi jioni Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Ngassa alisema, alfajiri aliondolewa na daktari wa timu hiyo, Edward Bavu aliyemshauri kwenda kupatiwa matibabu.

“Sitakuwepo sehemu ya kikosi kinachotarajiwa kucheza na Ruvu ni baada ya kuugua ghafl a malaria na kupelekea daktari kushauri nitolewe kambini kwa ajili ya matibabu.

“Baada ya kuondolewa kambini niliendelea na matibabu, lakini nashukuru naendelea vizuri kidogo kilichobaki ni kichwa pekee ambacho kinanigonga sana,”alisema Ngassa.
Ngassa aondolewa kambini Yanga Ngassa aondolewa kambini Yanga Reviewed by Zero Degree on 5/15/2019 05:08:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.