Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumapili Mei 19, 2019
Meneja wa klabu ya Chelsea ya wanawake Emma Hayes anataka kibarua cha Maurizio Sarri - kama atafukuzwa kwenye majira ya joto.
Tottenham wako tayari kuitibulia Everton dili la usajili wa Andre Gomes, ambaye anakadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 25.
Wolves wanafanya mazungumzo na mshambuliaji wa West Brom Salomon Rondon.
Asmir Begovic anaweza kufanya uamuzi wa kushitukiza kurejea Stoke wakati Bournemouth watakapojaribu kumsajili golikipa wa klabu hiyo Jack Butland.
Arsenal wako tayari kufanya jaribio la kumsajili mshambuliaji wa Lorient Alexis Claude-Maurice.
Manchester City na Liverpool wameungana na vilabu vinavyofuatilia saini ya chipukizi wa Inter Milan, Sebastiano Esposito.
Aston Villa tayari wanafanya maandalizi ya mazungumzo ya kuwasajili moja kwa moja Tammy Abraham, Tyrone Mings na Axel Tuanzebe wamaoitumikia klabu hiyo kwa mkopo.
Celtic wanapanga kumsajili chipukizi wa klabu ya Chelsea Fikayo Tomori kwenye majira ya joto.
Dennis Bergkamp ameziweka macho juu klabu za Uingereza baada ya kudai kuwa yuko tayari kurejesha mapenzi yake na EPL.
Middlesbrough wana nia ya kumsajili winga wa klabu ya Den Haag Sheraldo Becker, huku Mholanzi huyo akitarajia kumaliza mkataba wake kwenye majira ya joto.
Bristol City wanatarajiwa kumsajili kiungo mshambuliaji Sammie Szmodics kutoka Colchester United. (Mirror)
Klabu ya Manchester United imemwambia Paul Pogba kuwa ni lazima atume maombi ya uhamisho kama anataka kutimiza ndoto zake za kujiunga na Real Madrid.
Paul Pogba |
Mwanasheria wa Antoine Griezmann atakutana na klabu ya Barcelona wikendi hii kukamilisha taatibu za uhamisho wake wa pauni milioni 108 kutoka Atletico Madrid.
Pep Guardiola anapewa nafasi kubwa ya kumsajili kiungo wa Atletico Madrid Rodrigo - kama Man City wako tayari kumwachia Gabriel Jesus.
Chelsea watafukuzia saini ya nyota wa klabu ya Ajax David Neres, ambaye anakadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 40 kama watafunguliwa kutoka kwenye kifungo cha kufanya usajili.
Chelsea watawaacha Tammy Abraham na Kurt Zouma waendelea na mikataba msimu ujao kama adhabu yao itaendelea.
Crystal Palace wanamfuatilia mshambuliaji raia wa Colombia Duvan Zapata kama Christian Benteke ataondoka.
Arsenal watajaribu kumsajili nyota wa klabu ya Crystal Palace Wilfried Zaha kwa pauni milioni 40 badala ya 80, ambazo zimetajwa na klabu hiyo.
AC Milan wanapanga kumsajili beki wa klabu ya Arsenal Shkodran Mustafi kwenye majira ya joto.
Beki wa klabu ya PSG Dani Alves anatarajia kupokea ofa kadhaa kutoka vilabu vya Ligi Kuu ya Uingereza kwenye majira ya joto baada ya ofa zilizopita kutoka Manchester City na Manchester United.
Sheffield United wako tayari kutoa ofa ya pauni milioni 12 kumnasa Oli McBurnie - lakini wanakumbana na ushindani kutoka Brighton. (Sun)
Tottenham watalazimika kumpa meneja wa Juventus Massimiliano Allegri uhakika wa bajeti nzuri ya usajili kama watamtaka achukue nafasi ya Mauricio Pochettino.
PSG wako tayari kumpa David de Gea moyo wa kumaliza mkataba wake Manchester United na ajiunge nao kama mchezaji huru.
Unai Emery atajaribu kumsajili beki wa kati wa klabu ya Roma Kostas Manolas anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 31.
Manchester United wamejiunga na Barcelona pamoja Manchester City katika mbio za kuwania saini ya nyota wa Ajax Matthijs de Ligt. (Express)
Manchester United wanatazamia kumsajili golikipa wa klabu ya Ajax, Andre Onana kama mbadala wa David de Gea. (Record)
Manchester United wanaamini wana uwezo wa kumbakisha Marcus Rashford Old Traford kwa kuongeza mshahara wake hadi pauni 300,000 kwa wiki.
Mauricio Pochettino anawindwa na mabingwa wa Ligi Kuu ya Ujerumani Bayern Munich.
Chelsea wana nia ya kuwasajili Marco Asensio na Edinson Cavani, ikiwa adhabu yao itafutwa kwenye majira ya joto.
Real Madrid wanajiandaa kumnasa mshambuliaji wa klabu ya Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang. (Star)
Manchester City wataachana na nyota kadhaa ili kuwasajili Harry Maguire na Aaron Wan-Bissaka kwenye majira ya joto. (Times)
Chelsea watampa Callum Hudson-Odoi jezi namba 10 itakayochwa na Eden Hazard kwenye msimu huu wa majira ya joto, ikiwa ni mbinu ya kumshawishi asaini mkataba mpya.
Tottenham wanatarajiwa kushindana na Juventus kuwania saini ya kiungo wa klabu ya Lyon Tanguy Ndombele anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 87 kwenye msimu huu wa majira ya joto. (Sunday Mail)
Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumapili Mei 19, 2019
Reviewed by Zero Degree
on
5/19/2019 07:50:00 AM
Rating: