Loading...

ATCL kuanza safari za Johanesburg kesho


KAMPUNI ya Ndege Tanzania (ATCL) inazindua safari ya kwanza kwenda Johanesburg, Afrika Kusini kesho. Akizungumzia uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Ladislaus Matindi alisema hatua hiyo ni mafanikio ya mpango mkakati wao ulioanza mwaka 2017, waliojiwekea kuhakikisha shirika hilo linapata mafanikio kwenye usafiri wa anga kwa kufungua vituo vingi vya biashara nje ya nchi.

Matindi alisema safari katika ruti hiyo itahusisha ndege mpya za kisasa za Air- bus A220-300. Uzinduzi wa tiketi kwa ajili ya safari hiyo ulifunguliwa rasmi mwezi mmoja uliopita. “Nitoe mwito tu kwa Watanzania na wasafiri wote wanaokwenda kwenye majiji ya Johannesburg, Mumbai, Comoro, Zimbabwe na nchi nyingine tulikozindua safari zetu, wapande ndege za ATCL watafurahia huduma na bei zetu nafuu,” alisema Matindi.

Alisema kufunguliwa kwa kituo cha ndege za ATCL, jijini Johannesburg na kingine kitakachozinduliwa mwezi ujao Mumbai, India kunafanya idadi ya vituo vya biashara nje ya nchi kwa ndege hizo kufika saba. Vituo hivyo ni Zam- bia, Zimbabwe, Uganda, Comoro, Burundi, Johannes- burg na Mumbai.

Mapema mwezi uliopita, Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini India, ilitoa kibali kwa ATCL kuanzisha safari zake nchini humo ambapo Julai 17, mwaka huu kampuni hiyo itazindua safari zake kwenda Mumbai, India, huku dirisha la tiketi likiwa limeshafunguliwa. Hata hivyo, safari za nje ya nchi kwa ndege za ATCL zilichelewa kuanza kutokana na mambo ya msingi yaliyokuwa yakifanywa, ikiwemo nchi kurudishwa katika Jumuiya ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga (IATA).

“Tulipanga kuzindua mapema safari za nje, ila tulichelewa kwa sababu ya kukamilisha mambo ya msingi yaliyohitajiwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga (IATA) ambayo kwetu kwa sasa tumeshafikia mwisho,” alisema Matindi.

Kwa sasa ndege za ATCL zinafanya safari za kwenda Zambia, Zimbabwe na Uganda na ruti za ndani ya nchi kwenye mikoa kadhaa ikiwemo Kilimanjaro, Mwanza, Iringa, Mbeya na Zanzibar. Wakati huo huo, maan- dalizi ya kwenda safari nyingine za nje ya bara la Afrika ikiwemo Thailand, China kwa ndege ya Dream- liner na Airbus 220-300 yanaendelea.

Chanzo: Habari Leo
ATCL kuanza safari za Johanesburg kesho ATCL kuanza safari za Johanesburg kesho Reviewed by Zero Degree on 6/27/2019 08:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.