Kahata avunja ukimya Simba
Kahata anayeitumikia Kenya kwenye michuano hiyo inayoendelea nchini Misri, amekuwa akihusishwa kutakiwa na Simba tangu kabla ya msimu wa 2018/19 haujaanza.
Kiungo huyo wa Gor Mahia amesema tayari amekutana na viongozi wa Simba na kujadili suala hilo, lakini amewasubirisha mpaka Afcon itakapomalizika. “Nina ofa nyingi, miongoni mwa hizo ni kutoka Simba. Wamekuwa wakinifukuzia tangu msimu uliopita, lakini bado sijasaini kutokana na kwamba nina mkataba na Gor Mahia,” alisema Kahata.
Kahata avunja ukimya Simba
Reviewed by Zero Degree
on
6/26/2019 07:35:00 AM
Rating:
Reviewed by Zero Degree
on
6/26/2019 07:35:00 AM
Rating:
