Loading...

Kinachoendelea kwa mwanamke aliyempika supu mtoto


Mwanamke aliyefanya tukio la aina yake Mkoani Geita, anayejulikana kwa jina la Happines Shadrack (36), aliyemchinja mwanaye kisha kumkatakata vipande na kumpika supu, anatarajiwa kufikishwa mahakamani pindi upelelezi utakapokamilika.

Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa polisi Mkoa wa Geita Mponjoli Mwabulambo, ambapo amesema Jeshi la Polisi bado linaendelea na uchunguzi ili kubaini kama kosa hilo alitenda kwa kukusudia, na atafikishwa Mahakamani kwa kosa la mauaji.

''Bado tunamshikilia ili kubaini mambo mbalimbali na uchunguzi utakapokamilika tutampeleka mahakamani, na kesi yake inahusu mauaji na unajua kesi hizi huwa hazipelekwi katika Mahakama za kawaida huwa zinapelekwa Mahakama kuu''. - Ameeleza.

Tukio hilo lilitokea Juni 23 mwaka huu, katika kijiji cha Bulige kata ya Senga Mkoani Geita, ambapo alimpika supu mwanaye wa kumzaa Martha Yakobo (1).
Kinachoendelea kwa mwanamke aliyempika supu mtoto Kinachoendelea kwa mwanamke aliyempika supu mtoto Reviewed by Zero Degree on 6/27/2019 07:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.