Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya leo Alhamisi Juni 27, 2019


Manchester United imejiondoa katika harakati ya kutaka kumsaini beki wa Leicester na Uingereza Harry Maguire baada ya kuambiwa kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 atagharimu pauni milioni 100.

Bayern Munich imefanya mazungumzo na Paris St-Germain na ajenti wa mshambuliaji wa Ufaransa Ousmane Dembele kuhusu uhamisho wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22. (Mirror)

Mkufunzi wa klabu ya Nice nchini Ufaransa Patrick Vieira, 43, Mkufunzi wa klabu ya Rangers Steven Gerrard, 39, kocha wa Manchester City Mikel Arteta, 37, wameorodheshwa miongoni mwa wakufunzi wanaotarajiwa kumrithi Rafael Benitez. (Telegraph)

Raia wa Uhispania Mikel Arteta ameungwa mkono kuchukua ukufunzi wa klabu ya Manchester City wakati kocha Pep Guardiola atakapoondoka katika klabu hiyo.

Beki wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 19 Sepp van den Berg, anatarajiwa kujiunga na Liverpool kutoka kwa klabu ya PEC Zwolle. (Evening Standard)

Mkufunzi wa klabu ya Burnley Sean Dyche pia analengwa na Newcastle lakini the Magpies watalazimika kuwalipa Burnley £10m kama fidia. (Daily Mail)

Manchester United itakutana na ajenti wa kiungo wa kati wa Portugal Bruno Fernandes, 24, ili kujaribu kumrai kuhamia katika klabu hiyo kwa dau la £70m kutoka klabu ya Sporting Lisbon. (O Jogo)

Paul Pogba, 26

Juventus imeitaka kampuni ya vifaa vya michezo Adidas kuisaidia kifedha ili kuweza kumsaini kiungo wa kati wa klabu ya Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 26. (Corriere dello Sport)

Manchester City iko katika mzungumzo na Juventus kuhusu usajili wa beki wa kulia wa Ureno Joao Cancelo. (Tuttomercato)

Kiungo wa kati wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Uruguay Lucas Torreira, 23, anasema kuwa AC Milan haijawasiliana naye kuhusu uhamisho katika klabu hiyo ya Serie A. (Talksport)
Tetesi za soka barani Ulaya leo Alhamisi Juni 27, 2019 Tetesi za soka barani Ulaya leo Alhamisi Juni 27, 2019 Reviewed by Zero Degree on 6/27/2019 07:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.