Loading...

Wanaotumia vyeti feki vya kuzaliwa waonywa

Ofisi ya Idara ya Uhamiaji Kagera

Idara ya uhamiaji nchini imetoa onyo kwa raia wasio Watanzania ambao wanaishi hapa nchini kwa kutumia vyeti feki vya kuzaliwa, na kuwa wakibainika watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwamo kukamatwa na kufikishwa mahakamani.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za idara hiyo mkoani Kagera, Kamishna wa Udhibiti na Usimamizi wa Mipaka nchini, Samwel Mahilane amewatahadharisha watu hao kuwa wasijione wako salama kutokana na kuishi hapa nchini kwa muda mrefu, lakini uhakiki ukifanyika watagundulika.

Kauli hiyo imekuja baada ya kukamatwa kwa raia mmoja wa Rwanda, Budugu Dudagali Sekalomba, aliyekuwa akitumia cheti cha kuzaliwa alichouziwa na Francis Izaya Makala, ambaye inadaiwa alikwishaondoka hapa nchini.

"Wasitumie vyeti vya watu wengine, kwa sababu sisi tukihakiki ndio tutatambua mhusika mwenyewe kwahiyo niwammbie tu kuwa wataingia hasara, watalia na tutawashtaki", amesema Samwel Mahilane.

Aidha kamishna huyo ametumia fursa hiyo kuwaonya raia wasio wa Tanzania ambao watajipenyeza kuingilia uchanguzi wa serikali za mitaa kuwa watakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
Wanaotumia vyeti feki vya kuzaliwa waonywa Wanaotumia vyeti feki vya kuzaliwa waonywa Reviewed by Zero Degree on 9/27/2019 08:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.