30 wafa kwa ajali ya basi DRC, 18 wajeruhiwa
Ajali hiyo ilitokea jana Jumapili Oktoba 20, 2019 Mashariki mwa mji mkuu wa Kinshasa ambapo baadhi ya abiria waliokolewa na wengine kupata majeraha madogo.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Al Jazeera, basi hilo lilikuwa limebeba abiria 100 na Shirika la Msalaba Mwekundu lilikuwa likiendelea na uokozi katika eneo la tukio.
Msemaji wa shirika la Msalaba Mwekundu, David Nsiala alinukuliwa na Al Jazeera akisema wanaendelea kuitambua miili ya waliofariki kwenye ajali hiyo.
“Idadi ya vifo kwa sasa ni 30, wengine 18 wameungua sehemu kubwa ya miili yao,” alisema Nsiala ambaye anasimamia eneo la Mbanza – Ngungu, kama alivyonukuliwa na Shirika la Habari la AFP. Basi hilo lililokuwa limebeba abiria na mizigo lilikuwa linatoka Lufu kwenda Kinshasa kabla ya breki zake kufeli na kusababisha basi hilo kukosa udhibiti na kuanguka.

Abiria mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Nacha alisema basi hilo lilikuwa na abiria zaidi ya 100 na baadhi ya miili iliunguka kiasi cha kutotambulika.
Mbanza – Ngungu ni eneo lililopo kilomita 150 Mashariki mwa Kinshasa katika barabara kuu ambayo ina sifa ya kuwa na ajali nyingi ambazo zinasababisha vifo vya watu.
Mbanza – Ngungu ni eneo lililopo kilomita 150 Mashariki mwa Kinshasa katika barabara kuu ambayo ina sifa ya kuwa na ajali nyingi ambazo zinasababisha vifo vya watu.
30 wafa kwa ajali ya basi DRC, 18 wajeruhiwa
Reviewed by Zero Degree
on
10/21/2019 08:35:00 AM
Rating: