Loading...

ACT yazungumzia Membe kugombea 2020


Uongozi wa chama cha ACT-Wazalendo umezungumzia juu ya taarifa za kutaka kumpa nafasi Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika awamu ya nne, Bernard Membe katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2020.

Akizungumzia kuhusu suala hilo, Katibu Mwenezi wa chama hicho, Ado Shaibu amesema kuwa chama chake hakitasita kuungana naye endapo atahitaji lakini suala la kugombea ni mpaka mkutano mkuu utakapokaa na kuidhinisha.

"Membe ni mwanasiasa mashuhuri na anayejiamini licha ya zama hizi kutawaliwa na hofu. Ni aina ya mwanasiasa ambaye hakuna Chama chochote makini hakitamuhitaji", amesema Ado.

"Milango iko wazi kwake kujiunga ACT Wazalendo. Chama hiki kiliundwa ili kiwe "mbadala wa uhakika" kwa waliochoshwa na vyama vyao na wanaotaka kuendelea kupambana. Hivyo milango iko wazi kujiunga, lakini kuhusu Urais, Mkutano Mkuu utaamua. Inaweza kuwa Membe (akijiunga), Zitto au mwingine yeyote ambaye watu hawamjui bado. Wakati ukifika vikao vitaamua", ameongeza.

Chanzo: Eatv
ACT yazungumzia Membe kugombea 2020 ACT yazungumzia Membe kugombea 2020 Reviewed by Zero Degree on 10/21/2019 07:00:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.