Loading...

Chama mambo safi Simba SC


KIUNGO Mzambia wa Simba, Cletus Chama amemaliza tofauti yake na uongozi wa klabu yake hiyo na sasa yuko huru kuitumikia timu yake.

Chama alirejea nchini wiki iliyopita akitokea Zambia alikokwenda kuitumikia timu yake ya Taifa iliyocheza mechi dhidi ya Benin Jumapili iliyopita na kupata matokeo ya sare na mabao 2-2.

Kwa mujibu wa taarifa ya Dimba, kiungo huyo jana alikutana na Afisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, Senzo Mazingiza na kumaliza tofauti iliyokuwepo kabla ya kuruhusiwa kujiunga na wenzake.

Wachezaji kadhaa Simba akiwemo Chama, Erasto Nyoni, Gadiel Michael na Gerald Mkude wanakabiliwa na matukio ya utovu wa nidhamu baada ya kushindwa kuandamana na timu kwenda Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kucheza mechi mbili za Ligi Kuu.

Sakata hilo sasa limebaki wa Mkude, Nyoni, na Gadiel ambao walirejea jana na kikosi cha timu ya Taifa iliyokuwa nchini Sudan kucheza mechi dhidi ya timu ya Taifa ya nchini humo.

Kiongozi mmoja wa Simba aliliambia Dimba jana kwamba, baada ya Chama kumalizana na uongozi Mazingiza pia alitaka kukutana na akina Nyoni leo Jumapili.

Hata hivyo anasema, wachezaji hao wote wameshapewa taarifa ya kuhitajika na uongozi iliyobaki ni jukumu lao kutimiza ahadi au la.
Chama mambo safi Simba SC Chama mambo safi Simba SC Reviewed by Zero Degree on 10/21/2019 06:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.