Rais Magufuli awaapisha viongozi wapya serikalini
Hafla ya uapisho huo imefanyika katika Ikulu Jijini DSM.
Walioapishwa ni Mathias Kabunduguru ambeye ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama Tanzania,Godfrey Mweli kuwa Naibu mkuu Temisemi na Ali Sakila kuwa Balozi.
Akizungumza muda mfupi baada ya kuapishwa kwa viongozi hao Bw. Magufuli aliwataka watekeleza wajibu wao kwa kuzingatia sheria.

''Naibu Katibu Mkuu Temisemi ukaangalie maslahi ya waalimu hakuna sababu ya walimu kulalamika, Kashirikiane na waziri kusimamia wizara hii'', alisema
Hapo jana Jumamosi taarifa kutoka Ikulu ya Tanzania na kutiwa saini na Mkurugenzi wa Mawasiliano katika Ikulu ya rais, ilisema kuwa walioteuliwa ni Mathias Kabunduguru ambaye sasa ndiye mtendaji mkuu wa mahakama ya Tanzania, akichukua nafasi ya Hussein Katanga aliyeteuliwa kuwa balozi.
Wengine walioteuliwa ni Godfrey Mweli kuwa naibu katibu mkuu Tamisemi anayeshughulikia elimu.
Kabla ya uteuzi huo Mweli alihudumu kama mkurugenzi wa mipango katika wizara ya katiba na Sheria.
Hashim Abdallah Komba naye ameteuliwa kuwa mkuu wa Wilaya ya Nachingwea. Kabla ya Uteuzi huo Komba Komba alikuwa akihudumu kama katibu tawala mkoa wa Iringa.
Anachukua nafasi ilioachwa na Rukia Muwango ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Vilevile kiongozi huyo wa taifa amemteua Hassan Abbas Rungwa kuwa mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Nachingwea. Anachukua mahala pake bakari Mohammed Bakari ambaye ameondolewa na huenda akapatiwa kazi nyengine.
Licha ya kwamba hakutoa sababu za kuwapiga kalamu maafisa hao, akiwa ziarani mkoani Lindi aliwaonya viongozi hao kwa kushindwa kutimiza wajibu wao ipasavyo kulingana na gazeti la mwananchi nchini Tanzania.

Reviewed by Zero Degree
on
10/20/2019 11:35:00 AM
Rating: