Loading...

AS Roma yazindua ukurasa wa Twitter kwa lugha ya Kiswahili


Klabu ya mpira ya 'As Roma' nchini Italia imekuwa klabu kubwa ya kwanza kutoka barani Ulaya kuanzisha ukurasa wake katika mtandao wa Twitter.

Kurasa hiyo ya As Roma itakuwa ikiandika habari zake kwa lugha adhimu ya kiswahili.

Ukurasa huo wa lugha ya kiswahili ulizinduliwa rasmi jana, na inaaminika lengo kuu la 'As Roma' ni kuwafikia mamilion ya watu wanaotumia lugha ya kiswahili.

Akaunti hiyo ya Twitter imezinduliwa siku ya jumatano kwa video yenye maneno ya utani ya kiswahili.

Akaunti hiyo imepokelewa vizuri na wasomaji wa kiswahili wa Tanzania na Kenya.

Wengi wakiona kuwa ni ubunifu mzuri ambao unaonesha kuwajali mashabiki wanaoongea lugha ya Kiswahili.

Idadi kubwa ya watu wameanza kufuatilia kurasa hiyo na kujibu kwa kiswahili.


Rais wa klabu hiyo Jim Pallotta ametumia kurasa yake binafsi ya tweeter kuthibitisha kuwa kurasa hiyo imefunguliwa.

"Tuna furaha kuzindua kurasa ya kiswahili ya AS Roma", mkuu wa mipango Paul Rogers alieleza.


Uzinduzi huo umekuja mara baada ya kuzinduliwa kwa akaunti ya Pidgin.

Uzinduzi huu umekuja baada ya maombi ya mashabiki kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Afrika ya kati na mataifa mengine ya mashariki na kusini mwa Afrika.

Mapenzi ya soka la ulaya kutoka ukanda huu wa Afrika unastaajabisha kwa nini klabu za mpira za nje ya bara hilo kushindwa kuwasiliana kwa lugha ya kiswahili au Pidgin kabla ya mitandao ya kijamii.

"Kurasa hii ya Twitter itaturahisishia mawasiliano ya moja kwa moja na mashabiki wetu kwa namna ya kwao, ni mkakati ambao tunataka kuondoa vizuizi".

Akaunti mpya ya kiswahili ya AS Roma inawasiliana kwa lugha 14 tofauti katika mitandao ya kijamii.
Kuna kurasa nyingine rasmi za lugha ya kiitaliano, kiingereza, kiarabu,kifaransa, kireno, kichina, lugha ya Uturuki, Bosnian, , Dutch, Farsi na Pidgin.
AS Roma yazindua ukurasa wa Twitter kwa lugha ya Kiswahili AS Roma yazindua ukurasa wa Twitter kwa lugha ya Kiswahili Reviewed by Zero Degree on 10/17/2019 08:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.