Loading...

Barcelona yapata mbadala wa Luis Suarez


Mabingwa wa Ligi Kuu ya Uhispania wanajiandaa na maisha ya soka bila mshambuliaji raia wa Uruguay Luis Suarez.

Huku Suarez akiwa na umri zaidi ya miaka 30, Krzysztof Piatek anaweza kuwa chaguo la Barcelona kwa huduma ya muda mrefu.

Barcelona wameripotiwa kumtaja mshambuliaji wa klabu ya AC Milan Krzysztof Piatek kama mchezaji pekee anayestahili kuchukua nafasi ya Luis Suarez. Wakati raia huyo wa Uruguay akiendelea kubakia kuwa chaguo la kwanza la Ernesto Valverde, kumekuwa na uvumi unaozungumzia hatima ya nyota huyo pale Camp Nou.

Mshambuliaji huyo akiwa na umri wa miaka 32 sasa na mkataba unaotaajiwa kuisha mwaka 2021, Calciomercato linadai kwamba Barcelona wameanza kufikiria kutafuta mbadala wake. Ripoti hiyo inadai kwamba Piatek ameingia kwenye fikra zao, huku nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 akiwa tayari amekwisha kufunga mabao 11 katika michezo 24 ya Serie A tangu aelekee San Siro mwanzoni mwa mwaka

Barcelona tayari wameonyesha nia ya kutoa kiasi cha pauni milioni 44.5 kukamilisha usajili wake. AC Milan wanaweza kuhitaji zaidi ya kiasi hicho, licha ya kiwango chake kushuka kidogo, ambaye amefunga mabao mawili tu kwenye michezo sita ya ligi kuu ya Italia msimu huu. Suarez, Wakati huo huo, amefunga mabao matatu kwenye michezo yake sita msimu huu.

Krzysztof Piatek, 24


Piatek amebakiwa na pungufu ya miaka minne kwenye mkataba wake na vigogo hao wa Italia.

Ukiachana na nyota huyo, wapo wachezaji kadhaa waliotajwa kuwa miongoni mwa nyota wanaowaniwa na Barcelona kuchukua nafasi ya Suarez, akiwemo straika wa Juventus Mario Mandzukic, Timo Werner wa Leipzig na Jaime Mata wa Getafe.
Barcelona yapata mbadala wa Luis Suarez Barcelona yapata mbadala wa Luis Suarez Reviewed by Zero Degree on 10/03/2019 10:25:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.