Loading...

Beki Azam atamba kumdhibiti Meddie Kagere


BEKI wa timu ya Azam FC, Yakub Mohammed, ameanza kujiandaa kuwakabili washambuliaji hatari wa Simba akiwamo Miraji Athumani na Meddie Kagere.

Miraji na Kagere kwa sasa wanaonekana ni tishio kwa mabeki wa Ligi Kuu Tanzania Bara kutokana na uwezo wao wa kufunga mabao.

Katika michezo minne ambayo Simba imecheza, Miraji amefunga mabao matatu na Kagere akitupia wavuni mabao sita.

Kutokana na kasi ya washambuliaji hao wa Simba, beki huyo wa Azam FC amesema ameanza kujipanga kuhakikisha hawafungi bao wakati watakapokutana katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Oktoba 23, mwaka huu.

Beki wa Azam FC, Yakub Mohammed

Mohammed alisema pamoja na ubora wa Kagere, matarajio yake ni kuona hakatizi mbele yake.

“Mchezo wetu na Simba utakuwa mgumu lakini tutapambana, tunatambua ni timu kubwa yenye wachezaji wazuri kama kina Kagere,” alisema Mohammed raia wa Ghana.

Azam FC inashika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi wakiwa wamejikusanyia pointi tisa na hawajapoteza mchezo yoyote msimu huu sawa na Simba ambao wameshinda mechi zote nne na wapo kileleni wakiwa na pointi 12.
Beki Azam atamba kumdhibiti Meddie Kagere Beki Azam atamba kumdhibiti Meddie Kagere Reviewed by Zero Degree on 10/08/2019 01:20:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.