Loading...

Bobi Wine atajwa kuwa 'adui wa mafanikio' Uganda

Juhudi za Bobi Wine kuhamasisha Umma dhidi ya rais Yoweri Museveni zimekuwa zikizimwa na maafisa wa usalama

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amememtaja mkosoaji wake mwanamuziki aliyegeuka kuwa mwanasiasa Bobi Wine, kama "adui wa mafanikio ya nchi", 
Rais Museveni emeyasema hayo katika mahojiano na BBC.

Bwana Museveni anataka kugombea muhula wa sita kama rais mnamo mwaka 2021 baada ya kuwa rais wa nchi hiyo kwa miaka 33.

Bobi Wine, ambaye ni kiongozi wa vuguvugu la The People Power, anamshutumu rais huyo kwa kuongoza kwa mfumo wa ukandamizaji.

Bwana Museveni amekataa kumueleza mwandishi wa BBC Alan Kasujja ikiwa serikali yake ni ya ukandamizaji , lakini akasema anamshughulikia Bobi Wine kama adui.

Rais wa Uganda amesema ataendela kuwa madarakani zaidi ili kushughulikia matatizo ya Uganda na Afrika

Rais huyo wa Uganda amemlaumu Bobi akisema kwa kwenda Marekani na kusema kwamba watu wasije kuwekeza Uganda: ''Unapoenda na kuwaambia wageni kwamba hawapaswi kuja na kuwekeza katika nchi yetu, inamaanisha umeanzisha vita dhidi ya mafanikio yetu. Kwa hiyo ni kwanini sasa unataka kurejea na kunufaika na mafanikio hayo?". Amesema.

Hii huenda ndio moja ya sababu za kufutwa kwa matamasha ya muziki ya Bobi Wine, bado sijaongea na polisi kupata taarihfa zaidi, alisema.

Rais huyo wa Uganda anasema bado ataendelea kuwepo madarakani kwa miaka mingine zaidi kukamilisha kile ambacho yeye binafsi na wapiganaji wenzake walichokipanga kukifanikisha katika nchi yao na Afrika.

''Nyumba yangu inanisubiri, lakini tuna masuala kama Uganda ya kushughulikia.Ni masuala hayo ambayo yalitufanya tufanye kile tunachotaka kukifanya kisiasa pamoja na wenzetu. Kama chama tawala (NRM) kitafikiria kuwa hakihitaji mchango wa wazee badi tutaondoka madarakani kwa furaha na kufanya mambo mengine." Museveni alimueleza mwandishi wa BBC Allan Kasujja mjini Kampala.

''Hatupo hapa kwa ajili ya maonyesho, hatuendi kwenye ukumbi wa michezo ya maigizo , sisi ni watu ambao tupo hapa kushughulikia emasuala makubwa ya Uganda na Afrika." Alisistiza kiongozi huyo wa Uganda.

Rais Yoweri Museveni ambaye amekuwa madarakani Uganda sasa kwa zaidi ya miongo mitatu, amekuwa akikabiliwa na miito ya kumtaka ajiuzulu hasa kutoka kwa vijana na wapinzani wake akiwemo kiongozi wa upinzani Dkt Kizza Besigye pamoja na Mbunge Bobi Wine ambaye juhudi zake za kutaka kutumia usanii wake wa kimuziki kuhimiza ajiuzulu zimekuwa zikizimwa na maafisa wa usalama.
Bobi Wine atajwa kuwa 'adui wa mafanikio' Uganda Bobi Wine atajwa kuwa 'adui wa mafanikio' Uganda Reviewed by Zero Degree on 10/18/2019 11:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.