Loading...

Chanjo ya kifua kikuu mbioni kupatikana


Wanasayansi wamesema leo kuwa wanakaribia kugundua chanjo mpya ya ugonjwa wa kifua kikuu, ugonjwa hatari duniani ambao uliua watu milioni 1.5 mwaka jana.

Ugonjwa huo sugu wa mapafu unaotibika ulikuwa kati ya magonjwa 10 yaliyoongoza kwa kuua mwaka jana, hasa katika nchi zinazoendelea.

Chanjo iliyopo inayoitwa Bacille-Calmette-Guerin (BCG) --iliyoruhusiwa kutumika kwa binadamu mwaka 1921 -- imethibitishwa kutumika kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano tu na kwa aina chache za kifua kikuu.

Haikingi dhidi ya kifua kikuu kinachoanzia mapafuni (pulmonary TB) ambacho kinajulikana zaidi kwa watu wazima na vijana wadogo.

Katika majaribio yaliyofanyika nchi tatu za Afrika, kampuni ya GlaxoSmithKline ilisema chanjo hiyo ilikuwa na ufanisi wa asilimia 50 kw amiaka mitatu baada ya kupewa washiriki ambao tayari walishapata vijidudu vya kifua kikuu lakini hawakuugua ugonjwa huo.

"Matokeo hayo yanaonyesha kwamba kwa mara ya kwanza kwa karibu miaka mia, jumuiya ya dunia ina kifaa kipya cha kujilinda dhidi ya kifua kikuu," kiongozi wa GSK Vaccines, Thomas Breuer alisema katika taarifa iliyotolewa katika mkutano wa afya ya mapafu unaofanyika Hyderabad, India.

Wanaopigia kampeni sula hilo walisema majaribio nchini Kenya, Afrika Kusini na Zambia, yalkiyohusisha zaidi ya watu wazima 3,000, yalikuwa ni hatua muhimu katika kusukuma uchangiaji wa fedha za kufanya utafiti wa kifua kikuu.

Mkurugenzi wsa taasisi inayoshughulika na utafutaji wa chanjo ya kifua kikuu nchini Afrika Kusini, Mark Hatherill alisema chanjo hiyo itakuwa "njia pekee ya kuingilia uambukizaji kifua kikuu na kuudhibiti ugonjwa huo".

Ann Ginsberg, wa taasisi ya kimataifa inayoshughulikia utafutaji wa chanjo ya Ukimwi na ambayo imekuwa ikishiriki katika utafiti huo, ilisema chanjo 15 zinazoweza kuzuia ugonjwa huo, ziko katika hatua kadhaa duniani kote lakini lakini hiyo ndiyo iliyovutia zaidi.

Ikifanikiwa, chanjo hiyo itaweza kuzuia "mamilioni ya maambukizi ya ugonjwa wa kifua kikuu na kuokoa mamilioni ya maisha ya watu."
Chanjo ya kifua kikuu mbioni kupatikana Chanjo ya kifua kikuu mbioni kupatikana Reviewed by Zero Degree on 10/29/2019 09:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.