Loading...

Mtoto wa miaka 4 akutwa ameuawa nje ya nyumba mkoani Songwe

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe George Kyando

Hali ya taharuki imewakumba wananchi wa Mtaa wa Kwamwizya katika Mamlaka ya Mji Mdogo wa Vwawa Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, baada ya mtoto Nickson Mwaluanda wa miaka minne kukutwa amekufa akiwa ametupwa na watu wasiojulikana, kwenye mtaro wa nje ya nyumba ambayo walikuwa wakiishi.

Rehema Mwaluanda ni Bibi aliyekuwa akiishi na mtoto huyo, amesema mtoto huyo alikuwa amelala na wenzake wawili lakini watoto hao wamekuja kushtuka asubuhi mwenzao hayupo, huku milango ikiwa imefunguliwa.

Bibi huyo amedai hajui aliyemtoa mtoto nje na kumuua, kwani haikuwa rahisi kwa mtoto huyo kufungua milango yote, kwani nyumba yake ina milango miwili ya kutokea nje, mmoja wa chuma na mwingine wa mbao.

Kwa mujibu wataarifa ya Eatv, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe George Kyando, amethibitisha na kusema wanaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha kifo kama ni visa, kisasi au imani za kishirikina.
Mtoto wa miaka 4 akutwa ameuawa nje ya nyumba mkoani Songwe Mtoto wa miaka 4 akutwa ameuawa nje ya nyumba mkoani Songwe Reviewed by Zero Degree on 10/29/2019 08:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.