Loading...

Iran yatangaza sheria ya kutotembea


Waziri mkuu wa Iraq Adel Abdul Mahdi ametangaza sheria ya kutotembea nje katika mji mkuu Baghdad kuanzia mapema hii leo hadi kutakapotolewa taarifa nyingine.

Zuio hilo limetangazwa jana usiku kufuatia maandamano ya kitaifa ya siku mbili ya kuipinga serikali ambayo yalibadilika na kuwa ghasia. Tangazo la waziri mkuu huyo lilinukuu taarifa ya mkuu wa majeshi iliyozuia watu na magari kutembea mjini humo kuanzia saa 11 za alfajiri hii leo hadi taarifa nyingine itakapotolewa.

Wasafiri wanaoingia na kutoka kupitia uwanja wa ndege wa Baghdad, magari ya kubebea wagonjwa, watumishi wa serikali na hospitali, idara za umeme na maji pamoja na mahujaji wa kidini hawakujumuishwa kwenye katazo hilo.

Aidha, waziri mkuu Mahdi amewaambia magavana wa majimbo kuwa ni juu yao kuamua kuweka zuio hilo kwenye maeneo yao ama la.
Iran yatangaza sheria ya kutotembea Iran yatangaza sheria ya kutotembea Reviewed by Zero Degree on 10/02/2019 06:25:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.