Loading...

Lewandowski: Sijui habari za kwenda Real Madrid zinatokea wapi


STRAIKA wa Bayern Munich, Robert Lewandowski amezima tetesi zinazodai mwishoni mwa msimu huu atatimkia Real Madrid, baada ya mkataba wake na wababe hao wa Ujerumani kumalizika.

Staa huyo raia wa Poland amekuwa akihusishwa kujiunga na Real Madrid, lakini aliweka wazi mipango yake ya kuendelea kuwepo ndani ya kikosi cha mabingwa cha Ujerumani kinachonolewa na Nico Kovac.

“Sijui habari za kwenda Real Madrid zinatokea wapi, zinanishangaza, lakini kadri siku zinavyoenda nimekuwa nikizizoea.

“Inaonyesha jinsi gani mimi ni mchezaji mkubwa, mara kadhaa nimehusishwa na Madrid, Manchester United, Barcelona na Juventus, niseme ukweli, siwezi kuondoka hapa,” alisema.
Lewandowski: Sijui habari za kwenda Real Madrid zinatokea wapi Lewandowski: Sijui habari za kwenda Real Madrid zinatokea wapi Reviewed by Zero Degree on 10/01/2019 01:19:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.