Loading...

JPM aeleza sababu ya kumtumbua mkurugenzi NIMR


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jon Pombe Magufuli, amesema moja ya sababu kumtumbua aliyekuwa Mkurugenzi wa taasisi ya tafiti za kiafya NIMR, Mwele Malecela ni kiongozi huyo kutoa taarifa ambazo hazikuwa sahihi kuhusiana na ugonjwa wa Zika.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo akiwa mkoani Songwe, wakati alipofika kwenye ziara ya kikazi na kufanikiwa kuzindua kiwanda cha kahawa kilichojengwa na wajasiriamali Wakitanzania, ambapo amesema moja ya mambo ambayo yalipelekea kumtoa kwenye nafasi hiyo Mwele Malecelea ni kutangaza ugonjwa.

"Kuna wakati tulizushiwa tuna Zika Tanzania, yule aliyesema nikamfukuza saa 7 : 30 usiku, wala hakuna cha Zika, ikatokea baada ya wiki moja wakamteua akawa bosi wao." amesema Rais Magufuli

Kuhusiana na tukio la Mkuu wa Mkoa Mbeya kuwachapa wanafunzi katika Shule ya Sekondari Ikawanga mkoani Mbeya Rais Magufuli amepongeza suala hilo.

"Nampongeza RC Mbeya, ila kwa wale watoto walitimuliwa shuleni lazima wazazi wao walipe, nasema haya sio kwa sababu sina huruma nimeshawahi kuwa mwalimu, nawaomba wazazi nafikiri kuna mahali tumekosea ni sheria kuhusu viboko. amesema Rais Magufuli
JPM aeleza sababu ya kumtumbua mkurugenzi NIMR JPM aeleza sababu ya kumtumbua mkurugenzi NIMR Reviewed by Zero Degree on 10/05/2019 07:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.