Loading...

Samatta azungumzia sare dhidi ya Napoli


NAHODHA wa KRC Genk raia wa Tanzania, Mbwana Samatta, amefurahishwa na matokeo ya sare ya kutofungana dhidi ya Napoli ya Italia usiku wa kuamkia jana kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Genk ambayo ilifungwa mechi ya kwanza 6-2 na RB Salzburg ya Austria, ilionyesha mchezo mzuri dhidi ya Napoli inayofundishwa na aliyekuwa kocha mkuu wa Real Madrid na Chelsea, Carlo Ancelotti.

Akizungumza baada ya mechi hiyo, Samatta ambaye kwa mechi za hivi karibuni amekabidhiwa kitambaa cha unahodha, alisema Napoli haikuwa timu rahisi na walipambana kupata matokeo mazuri.

“Tulicheza dhidi ya timu ngumu, muhimu tumeonyesha ukomavu wetu, baada ya matokeo mabovu ya kwanza, tumeridhika na sare kila mmoja amefurahi,” alisema.

Mechi nyingine katika kundi la kina Samatta ilishuhudia Liverpool wakiifunga Salzburg 4-3. Licha ya sare hiyo ambayo imewapa pointi moja, Genk bado ipo nafasi ya nne Kundi E huku vinara wakiwa Napoli yenye pointi sita wakati Liverpool na Salzburg kila moja ana pointi tatu.
Samatta azungumzia sare dhidi ya Napoli Samatta azungumzia sare dhidi ya Napoli Reviewed by Zero Degree on 10/04/2019 10:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.