Loading...

JPM akubali jimbo la Nape lipewe hadhi mpya



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, ameagiza Halmashauri ya Lindi Vijijini, ibadilishwe na iitwe Halmashauri ya Mtama kwa kile alichokieleza kwamba, watendaji wengi wa Serikali kubaki mjini, kunachelewesha maendeleo kwa wananchi wanaoishi vijijini.

Rais Magufuli aliitoa kauli hiyo jana Oktoba 15, 2019, wakati akizungumza na wakazi wa Mtama, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake mkoani Lindi.

''Halmashauri hii haitaitwa tena ya Lindi Vijijini, itaitwa Halmashauri ya Mtama na haya maagizo niliyoyatoa, nitayatoa leo kwa Waziri Jafo wa TAMISEMI ili aweze kuyashughulikia kwa mujibu wa sheria'' amesema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli ametoa siku 15 kwa Halmashauri mbili, ikiwemo Korogwe na Bunda ili kuhakikisha wananzitatua kero alizozitatua leo mkoani Lindi, kabla ya huo muda alioutoa.
JPM akubali jimbo la Nape lipewe hadhi mpya JPM akubali jimbo la Nape lipewe hadhi mpya Reviewed by Zero Degree on 10/16/2019 07:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.