Loading...

Kauli ya Serikali kwa Gereza lililokumbwa na ukame


Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni, amelitaka Jeshi la Magereza kupeleka wataalamu katika Gereza la Kilimo na Mifugo Kitai mkoani Songea, ili kufanya tathmini ya utumiaji wa bwawa lililopo karibu na gereza hilo, ili kuondoa tatizo la ukame.

Naibu Waziri Masauni, ametoa kauli hiyo alipotembelea Gereza hilo ambalo ni moja kati ya Magereza kumi ya kimkakakati nchini yaliyoteuliwa kulisha wafungwa nchi nzima.

Naibu Waziri Masauni, amesema mkakati huo ni wa haraka ili kunusuru wafungwa kukosa chakula ikiwa ni sambamba na kutekeleza agizo la Rais John Magufuli la kutaka wafungwa waliopo Magereza wajitegemee kwenye chakula.

Awali akisoma taarifa ya Gereza hilo, Mkuu wa Gereza hilo Kamishna Msaidizi Dkt. Sylivesta Shija, amesema wamefanikiwa kulisha wafungwa katika Mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara.
Kauli ya Serikali kwa Gereza lililokumbwa na ukame Kauli ya Serikali kwa Gereza lililokumbwa na ukame Reviewed by Zero Degree on 10/28/2019 07:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.