Loading...

Pyramids yailaza Yanga CCM Kirumba


YANGA ambao ni wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya Kimataifa wana kazi ya kupindua meza mbele ya wapinzani wao Pyramids FC nchini Misri kwenye mchezo wa marudio utakaopigwa baada ya wiki mbili.

Ushindi wa mabao 2-1 walioupata wapinzani wao umeongeza uzito kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa leo uwanja wa CCM Kirumba.

Mchezo huo uliochezawa jana Oktoba 27 ulianza kwa kasi, huku Yanga ikikubali kwenda mapumziko ikiwa imefungwa bao 1-0.

Kipindi cha pili walianza kwa kasi bado mambo yalikuwa magumu kwa Yanga na kuwapa nafasi wapinzani wao kuandika bao la pili.

Mabadiliko ya kumtoa Mrisho Ngassa nafasi yake kuchukuliwa na Deus Kaseke pamoja na Juma Balinya kuingia akichukua nafasi ya Makame yaliongeza nguvu kwa Yanga.

Iliwachukua Yanga dakika 90 kuandika bao la kwanza kupitia kwa Papy Tshishimbi kwa shuti kali akimalizia pasi ya Kaseke.

Ili kusonga mbele Yanga itatakiwa kushinda mabao 2 ugenini na wanatakiwa kulinda lango lao lisitikiswe na wapinzani.

Itamkosa bekikisiki, Kelvin Yondan ambaye ameonyeshwa kadi nyekundu baada ya kuwa na kadi mbili za njano.
Pyramids yailaza Yanga CCM Kirumba Pyramids yailaza Yanga CCM Kirumba Reviewed by Zero Degree on 10/28/2019 07:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.