Loading...

Madrid wanapanga kumtumia Modric kumasa Christian Eriksen


Real Madrid wanaweza kumrejesha nyota wa Tottenham katika klabu hiyo ya kaskazini mwa London mwezi Januari.

Wala si Gareth Bale, bali ni Luka Modric ambaye inadaiwa anaweza kurejea Spurs muda wowote baada ya mwaka huu.

Real Madrid wanaripotiwa kuwa tayari kumtoa Luka Modric kama sehemu ya ofa kukamilisha usajili wa nyota wa Tottenham Christian Eriksen mwezi Januari. Raia huyo wa Denmark amekuwa mchezaji mwenye thamani kubwa kwa Spurs tangu ajiunge na klabu hiyo akitokea Ajax. Hata hivyo, mkataba wake wa sasa unamalizika mwakani kwenye majira ya joto na bado hajasiani mkataba mpya.

Kiungo huyo aliweka wazi lengo lake la kutaka kuondoka Tottenham kwenye majira ya joto, na Real Madrid wamekuwa wakihusishwa naye mara kwa mara. Uhamisho ambao haukuwahi kutokea, lakini nia ya Madrid bado haijafa.

Kulingana na El Desmarque, Real Madrid wanataka kumsajili Eriksen mwezi Januari na wako tayari kumtoa nyota wa zamani wa Tottenham Luka Modric kama sehemu ya ofa yao. Mkataba wa sasa wa nyota huyo wa timu ya taifa ya Croatia na klabu hiyo pia unamalizika mwakani kwenye majira ya joto na hadi muda huu bado hajasaini mkataba mpya.

Modric alifunga mabao 17 na kutoa 'assist' 27 katika michezo 160 ya michuano yote kuanzia 2008 hadi 2012.

Kabla ya kujiunga na Real Madrid, Modric alikuwa na wakati mzuri wa mafanikio Spurs, akifunga mabao 17 na kutoa 'assist' 27 kwenye michezo 160 ya michuano yote kuanzia 2008 hadi 2012. Madrid wanataka kumwachia Modric, pamoja na, kutwaa tuzo ya Ballon D’Or mwaka jana, lakini wanatambua kwamba kwa umri wake wa maiaka 34 hii ndio nafasi yao ya pekee kuachana naye na kupata faida kupitia yeye.

Anaweza asiwe mtu sahihi kuchukua nafasi ya Eriksen kwa sasa lakini uzoefu wa Modric unaweza kuwa na faida kwenye kikosi cha Maurico Pochettino. Hata hivyo, Spurs wanaweza kuhitaji kusajili kuingo mshambuliaji mwingine mwezi Januari anayefaa zaidi kuchukua nafasi ya raia huyo wa Denmark.
Madrid wanapanga kumtumia Modric kumasa Christian Eriksen Madrid wanapanga kumtumia Modric kumasa Christian Eriksen Reviewed by Zero Degree on 10/07/2019 09:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.