Magufuli amuagiza IGP Sirro kumsimamisha kazi kigogo polisi
Agizo la Urio aliyekuwa akikaimu nafasi ya kamanda wa polisi Mkoa wa Rukwa kusimamishwa kazi limetolewa leo Jumapili Oktoba 6, 2019 baada ya Rais Magufuli kumpigia simu Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro na kumtaka kumsimamisha kazi Urio.
Septemba 30, 2019 alipewa maelekezo ya kuwahamisha kazi askari tisa wa kituo cha polisi Laela kutokana na tuhuma za uonevu na kuomba rushwa lakini hakufanya hivyo.
Septemba 30, 2019 alipewa maelekezo ya kuwahamisha kazi askari tisa wa kituo cha polisi Laela kutokana na tuhuma za uonevu na kuomba rushwa lakini hakufanya hivyo.
Leo akiwa kwenye uzinduzi wa barabara ya Tunduma-Sumbawanga, Rais Magufuli alimuuliza kamanda wa polisi wa mkoa huo, Mathias Nyange kuhusu askari hao ila alionyesha kutofahamu chochote.
“Sina hayo majina na bahati mbaya sifahamu chochote sikuwepo ofisini aliyekuwepo hakunipa taarifa yoyote kuhusu maelekezo hayo,” amesema Kyando.
Baada ya majibu hayo Rais Magufuli alimpigia simu IGP Sirro na kumuagiza kumsimamisha kazi Urio.

“Nataka umsimamishe kazi na umshushe cheo maelekezo mengine nitakupa, anapewa maelekezo na waziri hataki kutekeleza, ” amesema Magufuli.
Chanzo: Mwananchi
Magufuli amuagiza IGP Sirro kumsimamisha kazi kigogo polisi
Reviewed by Zero Degree
on
10/06/2019 07:05:00 PM
Rating: